Saturday, July 25, 2015

CHUO CHA WAISLAM MOROGORO WASHIRKI MAONYESHO YA VYUO VIKUU

Chuo cha  Waislam Morogoro kimeshiriki maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2005 na mpaka sasa kina miaka 10 kinatoa kozi mbalimbali kwa wanafunzi wanaojiunga katika chuo hicho. Afisa mahusiano wa chuo cha Waislam Morogoro, Ngaja Mussa akimwonyesha Mkufunzi mkuu wa chuo cha Waislam Morogoro, Faraji Tamim wakati wa maonyesho ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu nyerere jinini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo hicho, Sun Xiaofei akizungumza na wateja mbalimbali waliotembelea katika maonyesho ya vyuo vikuu vya hapa nchini na nje ya nchi.
Afisa Udahili Yahya Mhando akitoa maelekezo kwa watu waliotembelea katika banda la Chuo cha Waislam-Morogoro katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya vyuo vikuu yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo  cha Waislamu Morogoro, Sun Xiaofei akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu walipotembelea katika maonesho ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments: