Monday, July 20, 2015

AIRTEL AZINDUA MNARA WA MAWASILIANO KIJIJ CHA NDURUMA MKOANI ARUSHA

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelis Lumato akikata utepe
kuzindua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
katika kijiji cha Nduruma, wilayani Arumeru Mkoani Arusha ,
akishuhudia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton
Majwala.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton Majwala akitoa msaada
wa vitabu  Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Singisi , Hamad
Boay , wakati wa uzinduzi wa huduma manara wa huduma za mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika kijiji cha Nduruma,
wilayani Arumeru Mkoani Arusha.  Shule zilizofaidika na msaada wa
vitabu ni pamoja na  sekondari za Nduruma na Singisi wilaya Arumeru.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua huduma za mawasiliano
ya simu za mkononi katika kijiji cha Nduruma wilayani Arumeru mkoani
Arusha na kuwawezesha wakazi zaidi ya 25,000 kupata huduma za
mawasiliano.

Katika uzinduzi huo , Airtel pia ilitoa msaada wa vitabu vya sayansi
kwa shule mbili za sekondari za Nduruma na Sing'isi,  vyenye jumla ya
thamani ya shilingi milioni 4.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton Majwala alisema" Uzinduzi huu ni
mwendelezo wa dhamira yetu unaoenda sambamba na mipango ya serikali ya  kutoa huduma za mawasiliano kwa kila mtanzania.

 Leo tunayofuraha  kuwawezesha wakazi wa vijiji vya Samaria, Majimoto na Maroran kupata huduma za mawasiliano za uhakika, zenye ubora na za gharama nafuu huku tukiwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa ufanisi zaidi"

"Tunaamini huduma hizi za mawasiliano zitachangia katika kuboresha
shughuli za kiuchumi zikiwemo ufugaji, kilimo  pamoja na biashara
ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi. Sasa wakazi wa Nduruma
wamewezeshwa kupata habari muhimu kupitia simu zao za mkononi wakati  wotote na kwa urahisi zaidi" 

Majwala aliongeza kwa kusema"  Sambamba na uzinduzi wa huduma za
mawasiliano pia tumeweza kutoa vitabu vya sayansi kwa shule mbili za
sekondari wilaya hapa ili kuwawezesha wanafunzi na jamii kupata elimu
bora. 

 Tunaamini vitabu hivi pamoja na huduma hizi za mawasiliano
zitachangia kwa kiasi kikubwa k kubadili maisha ya wengi na
kuwawezesha watanzania na wakazi wa hapa kuzifikia ndoto zao".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelis Lumato ambaye ndiye aliyezindua mnara huo na kutoa vitabu kwa shule za
sekondari alisema" tunayofuraha kupata huduma za mawasiliano kutoka
Airtel hapa Nduruma pamoja na vijiji vya jirani. Hii ni nafasi ya 
pekee kwa wakazi wa hapa kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kutumia mawasiliano haya katika kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kijamii" 

"Serikali itaendelea kuwaunga mkono Airtel katika jitihada zao za
kuhakikisha inatanua wigo wa huduma za mawasiliano na kufikia maeneo
mengi hususani yaliyo pembezoni mwa nchi. Nawapongeza sana kwa juhudi  hizi na kuwaasa wakazi wa hapa kutumia fulsa hii katika kujiendeza na kuleta maendeleo"

Kwa upande wake, Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Singisi ,
Hamad Boay alisema"  Tunashukuru sana Airtel kwa kutupatia msaada huu   wa vitabu ambao utaboresha uwiano wa vitabu na idadi ya watoto shule ambapo hapo awali kitabu kimoja kinatumika na wanafunzi watano, msaada huu utaboresha uwiano ambapo kwa sasa mwanafunzi mmoja atatumia kitabu kimoja.

Tunaahidi kuvitumia vizuri na kuvitunza lakini zaidi wanafunzi wetu
watafanya vizuri kimasomo na kutoa wanasayansi bora shuleni hapa."

No comments: