VIONGOZI WA KIMASAI WARIDHIA KUACHA UKEKETAJI
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) akimpongeza Kiongozi
Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli
kwenye semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi,
viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa
idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro.
Susana Koillah, Mama Shughuli na mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika
semina hiyo akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kulia) kabla ya kutafsiri mada yake kwa wanasemina.
Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi,
viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na
vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa wa Shirika la Kimataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Mathias Herman (kushoto)
akitoa maelekezo kwa wana semina ya viongozi wa jamii ya kimasai,
wazazi, viongozi shule za sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo
vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo
iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi,
viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na
vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
WAKUU wa jamii ya Kimasai wa Afrika Mashariki wameridhia kuachana
na mila potofu zimezopitwa na wakati ikiwemo vitendo vya ukeketaji kwa
wasichana wa jamii ya kimasai ambavyo vimekuwa vikiwaathiri wasichana
hao kwa kiasi kikubwa.
Kauli ya kusitisha
vitendo hivyo ilitolewa juzi Wilayani Ngorongoro na Kiongozi Mkuu wa
Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na
msaidizi wake kutoka Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni walipokuwa katika
semina ya elimu ya afya ya uzazi, kupinga vitendo vya ukeketaji pamoja
na mimba za utotoni.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya
Wamasai Afrika Mashariki, Olaiboni Simeli alimueleza Mkuu wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) na Mwakilishi wa
Shirika hilo Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues kuwa jamii hiyo ya wamasai
imeridhia kuacha mila zilizopitwa na wakati na itaendelea kushiriki
kuelimisha jamii yao zaidi juu ya madhara ya mila hizo potofu ikiwemo
ukeketaji na ndoa za utotoni.
"...Tunaishukuru
UNESCO kwa kuendelea kutoa elimu hii kwetu juu ya mila potofu nasisi
tunaungana nanyi kuendelea kutoa elimu kwa jamii yetu kupinga ukeketaji
na ndoa za utoto tumeelezwa athari nyingi zinazowapata wasichana
wanaokeketwa...kwanini tuendelee na mila zinazoleta madhara kwa watu
wetu? Tushirikiane kupiga vita hivi," alisema Olaiboni Simeli
akizungumza mbele ya Bi. Rodrigues.
Kwa upande
wake Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Naimado Olaiboni
alisema hakuna haja ya jamii ya kimasai kuendelea na mila zilizopitwa na
wakati ilhali mila hizo zikiendelea kuwaathiri wamasai na kuwabakiza
nyuma kimaendeleo katika nyanja mbalimbali. "...Tutaendelea kushirikiana
nanyi kupinga ndoa za utotoni kwa kuwa tumeelezwa madhara yake na
wataalamu leo," alisema Naimado Olaiboni.
Naye
Mkuu wa Shirika la UNESCO na Ofisa Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania,
Bi. Rodrigues alisema anapenda kuona Jamii ya Kimasai inaendeleza mila
na tamaduni zao lakini zile nzuri ambazo hazina chembe ya kiunyanyasaji
kwa makundi yote. Alisema ukeketaji kwa wasichanga unamadhara makubwa
kwa jamii hiyo hivyo haina budi mila hizo kupuuzwa ili kumlinda mtoto wa
kike na madhara yanayomkumba anapofanyiwa vitendo hivyo.
"...Napenda
kuona Wamasai wanaendeleza mila na tamaduni zao lakini ziwe nzuri na
zisizo na chembe ya ukatili wala unyanyasaji, tuangalie ni namna gani
tunaziendeleza na kubaki katika uhalisia wetu...nawahakikishia
tutashirikiana kuhakikisha hili linafanikiwa kwenu," alisema Bi.
Rodrigues akizungumza katika semina hiyo.
Aidha
aliwashauri jamii ya Kimasai kupunguza kuwa na idadi kubwa ya watoto na
wake ilhali mume akishindwa kuihudumia familia hiyo jambo ambalo
limeendelea kuchochea umaskini wa familia hizo vijijini kwani watoto
wamekosa mahitaji ya msingi katika familia na kujikuta wakiishi kwa
taabu.
Aliwataka Wamasai pia kupinga ndoa za
utotoni kwani mabinti wadogo wanapoolewa wanakosa fursa ya elimu pamoja
na kuunda familia bora kutokana na uduni wao katika masuala ya afya ya
uzazi kiujumla na madhara yanayowaandama katika maisha yao. "...Ndoa za
utotoni nazo ni tatizo katika jamii yetu, tuzipige vita maana mtoto
mdogo anapoolewa haweza kuunda familia bora na wala uzazi wake hauwezi
kuwa bora...," aliongeza Bi. Rodrigues.
Zaidi
ya wanasemina 210 kutoka Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu,
Oloipili, Aoliani Magaidulu wakiwemo viongozi mbalimbali wa jamii ya
kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari na wakuu wa
idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii Wilayani Ngorongoro
wamenufaika na semina hiyo ya jitihada za kuelimisha jamii juu ya mila
na desturi zilizopitwa na wakati.
Kutoka kushoto ni Mshauri na Mkufunzi wa Masuala ya Vyombo vya Habari
Jamii kutoka UNESCO Tanzania, Rose Haji pamoja na Mkuu wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi.
Zulmira Rodrigues wakifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na UNESCO juzi.
Baadhi ya washiriki wa semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya
kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa
idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro
wakifuatilia mada kwenye semina hiyo.
Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Emanyata Ololosokwani na Mwenyekiti
warsha hiyo, Ole Daniel akitafsiri kwa lugha ya kimasai mada ya Mkuu wa
Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini
Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) alipokuwa akiwasilisha.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) akimsikiliza Kiongozi
Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli
(kulia) kwenye semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai,
wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro,
wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya
Ngorongoro.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika
semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za
msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa
jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyoandaliwa na Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) wakichangia mada
mbalimbali.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika
semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za
msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa
jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Susana Koillah, Mama Shughuli na mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika
semina hiyo akisisitiza jambo. Kulia ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika
semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za
msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa
jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi,
viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na
vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni
(kushoto) akichangia mada katika semina ya viongozi mbalimbali wa jamii
ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani
Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya
ya Ngorongoro. Wengine ni wasaidizi wa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya
Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli wakishiriki semina
hiyo.
Baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania wakiwapongeza viongozi wa jamii ya
kimasai, Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo
Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania,
Sangau Naimado Olaiboni mara baada ya semina kumalizika.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni
Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau
Naimado Olaiboni wakipiga picha za kumbukumbu na baadhi ya maofisa
kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania baada ya semina kumalizika. Kulia ni Ofisa Mradi Elimu
wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini
Tanzania, Jennifer Kotta akijiandaa kuwapongeza viongozi wakuu wa jamii
ya kimasai Afrika Mashariki na Tanzania walioshiriki semina hiyo.
Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa wa Shirika la Kimataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Mathias Herman (kulia)
akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau
Naimado Olaiboni (kushoto) mara baada ya semina ya viongozi wa jamii ya
kimasai, wazazi, wakuu shule za sekondari, wakuu wa idara ya afya na
vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Imeandaliwa na www.thehabari.com, Ngorongoro .
No comments:
Post a Comment