Monday, June 22, 2015

AIRTEL FURSA "TUNAKUWAWEZESHA" YAMUWEZESHA FUNDI NGUO, BETHA BENEDICT MKAZI WA BUNJU JIJINI DAR

Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kukabdhi mashine ya cherehani yakushonea nguo kwa fundi wa kushona nguo, Betha Benedict mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” (katikati), Betha Benedict aliyewezeshwa na mpango huo, na kushoto ni mama yake Betha Benedict.
????????????????????????????????????Mama yake Betha akiishukuru Kampuni ya Airtel kwakumuwezesha Mwanae kwakupitia mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”
????????????????????????????????????Mratibu wa Chuo cha (MTCD) Dogodogo kinachotoa mafunzo kwa Vijana waishio katika mazingira magumu kuanzia Umri wa miaka 10-16, Bw.Issa Buzohera naye akishukuru Kampuni ya Airtel kwa mpango huo.
????????????????????????????????????Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (wa pili kulia ), akimkabidhi zawadi ya mashine ya kushonea ‘cherehani’, Betha Benedict (wa pili kushoto), mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakwezesha”. Kushoto ni mama yake Betha na kulia ni Meneja wa Airtel, Fadhili Mwasijeba.
????????????????????????????????????Betha Benedict akioneshwa na Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi vifaa vinavyotumika katika mashine ya kushonea nguo cherehani.
????????????????????????????????????Baada ya makabidhiano ikawa ni furaha kwa ,Betha pamoja na vingozi wa kampuni hiyo.
????????????????????????????????????Betha Benedict (kulia), akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Airtel mara baada ya kuwasili nyumbani kwake kwaajili ya kumkabidhi zawadi (katikati), Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi.
????????????????????????????????????Betha Benedict (kusoto) akisalimiana na Afisa Uhusiano na Matukukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati), mama yake Betha Benedict.
????????????????????????????????????Picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale
AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake mpya wa Airtel Fursa-Tunakuwezesha imemkabidhi kijana Betha Benedict vifaa
mbalimbali vya kushonea na mashine ya kushonea nguo ‘cherehani) ambavyo vitamsaidia katika biashara yake ya kushona nguo na kumuongezeaa kipato chake.

Betha ambaye ni mkazi wa Bunju alikabidhiwa vifaa hivyo juzi na Kampuni ya simu ya Airtel ambapo awali alikuwa akitumia cherehani kimoja na kuwa na changamoto ya ufanyaji wa kazi yake hiyo ya ushonaji.

Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi.

Alisema Betha amepitia changamoto nyingi kupitia kazi yake hiyo ya ushonaji kwani ndiye anayeitunza familia yao mama pamoja na wadogo zake hivyo fursa hiyo aliyoipata itamuwezesha asonge mbele kimaisha.

“Betha ni kijana wa pili kufaidika na mpango huu na kama tulivyosema hapo awali mpango huu unawalenga vijana ambao tayari wanajihusisha na miradi mbalimbali kama Betha na wanatakiwa kutuma maombi yao,” alisema na kusisitiza kuwa mpango huo hauwalengi wanaotaka kuanzisha miradi.

Alimtaka Betha atumie vifaa hivyo vizuri iliaweze kujiendeleza zaidi na kuwa mfano mzuri kwa vijana ili kuutangaza vizuri mpango huu.

Bayumi aliwataka vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.

“Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini,” alisema.
“Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma
ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com  mailto:airtelfursa@tz.airtel.com. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtelwww.airteltanzania.com http://www.airteltanzania.com/,”
alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062-0786-858550)

No comments: