Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita akikabidhi kombe kwa mabingwa timu ya MUcoba FC |
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita akikabidhi kombe kwa mabingwa timu ya MUcoba FC |
Mratibu wa kombe la Muungano Mufindi Daud Yassin akitangaza kustaafu nafasi yake hiyo |
Mabingwa wa mashindano ya kombe la Mungano Mufindi |
washindi wa pili wa mashindano ya kombe la Muungano Mufindi timu ya Dodoma Academ wakipita kuvishwa medali na Feisal Asas |
Mwalimu wa timu ya Mabingwa wa fainali ya Muungano Cup akipongezwa |
Na MatukiodaimaBlog
MASHINDANO ya kombe la Muungano Mufindi yamefikia tamati baada ya timu ya benki ya wananchi wilaya ya Mufindi (MUCOBA FC) kuibukwa mabingwa wa fainali ya mashindano hayo kwa kuigagadua (kuifunga) timu ya Academ kutoka Dodoma kwa jumla ya magoli 2-0
Huku mratibu wa mashindano hayo Daud Yassin akitangaza kustaafu rasmi nafasi yake hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 19 hivi sasa .
Mratibu huyo aliweza kuwaaga rasmi wapenzi wa mpira wa miguu katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa wa shule ya msingi wambi mjini Mafinga
. Yassin aliwashukuru wadau wote wa soka waliomsaidia kwa namna moja au nyingine kwa miaka 19 aliyoratibu mashindano hayo.
Alisema pia anawashukuru viongozi mbalimbali, chama cha soka wilaya ya Mufindi, chama cha soka mkoa wa lringa, shirikisho la soka nchi TFF, na ZFA kwa kuonyesha ukaribu wao kwa kipindi chote cha mashindano hayo .
Pia aliwaomba radhi wadau wote ambao walikwazika kwa utendaji wake endapo alikosea katika utendaji wake na kuwa haikuwa makusudi yake kuwakwaza .
Amesema kwa sasa hatajihusisha na mambo ya soka tena katika wilaya hiyo kwani kazi aliyoifanya kwa kipindi cha miaka hiyo 19 ni kubwa na wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa umetangazwa zaidi kupitia mashindano hayo .
" Nimejifunza mengi mwaka huu mambo yalikuwa magum sana japo anawashukuru wale waliomsaidia kufanikisha na kuwa atawaandikia rasmi kuwashukuru.....Wakiwemo viongozi wa kisiasa mbunge wa kaskazini Mahamudu Mgimwa na mjumbe wa NEC na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini kwa kumsaidia kufanikisha mashindano hayo kwa mwaka huu "
Mgeni rasmi katika fainali hiyo mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita mbali ya kumshukuru mratibu huyo wa kombe la Muungano Mufindi ,Yassin pia alipongeza wadau wote ambao wameyafikisha hapo mashindano hayo na kuwa wilaya ya Mufindi imeweza kutangazwa vilivyo kupitia soka .
Hivyo aliwataka wadau wa soka wilaya ya Mufindi kuangalia uwezekano wa kuendeleza mashindano hayo baada ya mratibu wake kustaafu rasmi na kuwa akiwa mkuu wa wilaya hiyo atahakikisha mashindano hayo yanaendelea japo ushauri wa mratibu huyo utaendelea kuhitajika zaidi.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza timu ya Mucoba Fc ilipata zaiwa ya kombe kubwa , pesa taslim kiasi cha Tsh milioni 5 ,jezi seti nne na medali ,wakati mshindi wa pili Dodoma Academ ikipata kiasi cha Tsh milioni 2.5 ,seti tatu za jezi pamoja na medali wakati mchezaji bora akipata kiasi cha Tsh 500,000
No comments:
Post a Comment