Monday, June 8, 2015

TASWIRA MBALI MBALI ZA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR, DKT. SHEIN NCHINI UJERUMANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa Gazeti la Main Post la Mjini Wurzburg Nchini Ujerumani baada ya kulitembelea jingo la Serikali linalotumika kwa kwa shuhuli mbali mbali ikiwemo shuhuli za Utalii rais na ujumbe wake alitembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Tropiki Prof.Dr.med.Augustin Stich baada ya Taasisi ya Tafiti mbali mbali yakiwemo magonjwa ya Binadamu, Chuo cha Afya katika Mji wa Wurzburg kimeweza kutoa mchango mkubwa katikakupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea Nchi za Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Mario Gerth (kulia) wakati waalipotembelea katika kituo cha maonesho ya picha Spitale katika Mji wa Wurzburg picha hizo zenye kuonesha Zanzibar na Ustaarabu wa Waswahili zilizotayarishwa chini ya nusimamizi wa Dr.Stefan Oschman Mkurugenzi wa Tamasha la Muziki wa Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Zanzibar Amber Resort Bi Naila Jidawi wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na sanaa za Mzanzibar katika viwanja vya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipa maelezo kutoka kwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Nd,Issa Mlingoti wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na sanaa za Mzanzibar katika viwanja vya maonesho 27 ya Muziki wa Afrika katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini na ujumbe nwake juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiangalia picha za ramani ya ujenzi wa Mradi wa Zanzibar Amber Resort Bi Naila Jidawi wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na sanaa za Mzanzibar katika viwanja vya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea kitabu cha ramani ya ujenzi wa Mradi wa Zanzibar Amber Resort kutoka kwa Msimamizi Mkuu Bi Naila Jidawi wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na sanaa za Mzanzibar ikiwemo mikoba ya ukili na kazi nyengine akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na ujumbe waliofuatana nao katika ziara ya kikazi maonesho yaliyofanyika juzi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani.
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd,Saleh Ramadhan Feruzi alipokuwa akitoa maelezo kwa wageni wakitalii mbali mbalio waliofika katika mabanda ya kazi mbali mbali kutoka Zanzibar wakati wa Maonesho ya Tamasha la 27 ya Muziki wa Afrika yaliyomalizika juzi katika viwanja vya Wurzburg Nchini Ujerumani ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinalipofanya ziara ya kikazi ya siku nane nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiangalia kazi mbali mbali za kiutamaduni wa Zanzibar ikiwemo kusuka ukili,mikoba na utiaji wa hina na wanja kwa watalii waliotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi hizo katika viwanja vya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo juzi.
Mchoraji wa mauwa kutumia wanja na hina akiwaremba watalii wakati wa maonesho ya 27 ya Tamasha la muziki wa Taarab kutoka Zanzibar pia Tamasha lilijumuisha wasanii mbali mbali wa fani hiyo kutoka nchi mbali mbali Duniani na kazi za kiutamaduni katika kuitangaza Zanzibar Kiutalii katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd,Saleh Ramadhan Feruzi walipoangalia kazi mbali mbali za uchoraji ikiwa ni katika hatua za kukuza Utalii wa Zanzibar katika mabanda ya maonesho ya Kazi hizo katika viwanja vya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Masoko Salum A.Kibe wakati walipoangalia bidhaa mbali mbali za karafuu ikiwa ni katika hatua za kukuza Utalii wa Zanzibar katika mabanda ya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani juzi akiwa katika ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa INAYA ZANZIBAR ni taasisi inayojishulisha na biashara ya uuzaji wa vipodozi kama sabuni ,mafuta ya kujipaka ambavyo vina asili ya Zanzibar vinavyotumika katika mahotelini na nyumbani wakati walipoangalia bidhaa mbali mbali zinazopelekea hatua za kukuza Utalii wa Zanzibar katika mabanda ya maonesho Mjini Wurzburg Nchini Ujerumani juzi akiwa katika ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na ujumbe waliofuatana nao walipokuwa akiangalia bishara zenye asili ya Utaduni wa Zanzibar ikiwemo mikoba ya ukili na kanga wakati walipomtembelea Mjasiriamali kutoka Zanzibar katika mabanda ya maonesho ya Kazi hizo katika viwanja vya maonesho Mjini Wurzburg Nchini Ujerumani juzi akiwa katika ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akibadilishana mawazo na Viongozi wa baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za maonesho ya Tamasha la 27 la Muziki ambapo Zanzibar ilishiriki kujitangaza kiutalii na kuonesha bidhaa mbali mbali katika maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Eneo maalum lililotengwa Mjini Wurzburg Nchini Ujerumani katika ziara ya kiazi ya siku nane nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake walipofika katika viwanja vya maonesho na kuwatembelea wasanii wa kikundi cha muziki wa Taarab cha Matona kutoka Zanzibar na kuwapa moyo katika jitihada zao za kuitangaza Zanzibar Kiutalii Nchini Ujerumani katika Tamasha 27 la Muziki katika ziara ya kiazi ya siku nane nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakiangalia wasanii wa kikundi cha muziki wa Taarab cha Matona kutoka Zanzibar wakitoa burudani kwa nyimbo mbali mbali wakiwa wamevalia mavazi ya asili ya Utamaduni katika viwanja vya maonesho katika kuitangaza Zanzibar Kiutalii Nchini Ujerumani katika Tamasha 27 la Muziki katika ziara ya kiazi ya siku nane(pichani) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein na Waziri wa Kilimo na Maliasili Sira Ubwa Mamboya wakitunza.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakifuatana na Dr.Stefan Oschman Mkurugenzi wa Tamasha la Muziki wa Afrika baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Zanzibar katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani katika hatua zakuitangaza Zanzibar kiutalii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akiwa na ujumbe wake wakiapata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa anaehusika na ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wake wakiangalia magari ya aina mbali mbali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa anehusika na Ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa na ujumbe wake wakiangalia mashine ya gari aina ya Mercedes -Benz na kupata maelezo kutoka kwa afisa anaehusika na ufundi Adam Nowak M.A katika kampuni hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Adam Nowak M.A. Afisa anaehusika na ufundi wakati alipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz akiwa na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani katika Mji wa Wurzburg ambaapo yapo tayari kwa mauzo.[Picha na Ramadhan Othman.]

No comments: