Monday, June 8, 2015

18 WATAJWA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015

Jopo la Majaji, Kutoka Kulia ni Zephaniah Muggitu wa Digital Consulting Ltd, Jairos Mahenge Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi  Oxfam akikaribisha majaji kwa ajili ya kutaja majina ya washindi watakao ingia shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015
 Mmoja wa majaji Zephaniah Muggitu  Akieleza kwa ujumla Jinsi mchakato wa kuwapata washindi hao ulivyokuwa
 Bi Dora Myinga ambaye pia alikuwa Jaji akisoma majina ya washindi 18 walioingia katika Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
 Mmoja wa Majaji Roselyn Kaihula  akielezea kuhusiana na jinsi fomu zilivyo chambuliwa na kupatikana washindi 18.
 Bi Mwandiwe Makame  akishukuru Juhudi za Serikali katika kuendeleza na kukuza kilimo
 Bw. Jairos Mahenge ambaye Pia alikuwa ni Mmoja wa Majaji akizungumzia kwa ufupi changamoto walizokutana nazo wakati wa Mchakato mzima wa kuhakiki fomu za kuwapata washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula.
 Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo mafupi ya Jinsi watakavyo watembelea washindi 18 katika maeneo walipo ili kuona shughuri zao na baadae kuwapata washiriki 15 ambao ndio wataingia katika mshike mshike wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015

*********
Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha fomu za washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 kukamilika, takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata mshindi.

akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki, Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.

Jaji huyo aliongeza kuwa fomu za washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi ya asilimia hamsini huku vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao ya chakula, uvuvi na ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za juu kutoka mikoa tofautitofauti.

Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania  Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote  watatembelewa maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli na baadae kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.

<![endif]-->Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie  L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi, Dina Samwel Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto Tanga, Edna Gabriel Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35) Hanang  Manyara,  Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva Mageni Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani  Mkata (56) Masasi Mtwara, Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida, Shida Daudi Mwedugo (35) Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini, Upendo Paulo Mhomisoli (35) Njombe, Savera  Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera, Carolina Humphrey Chelele (48)  Kilombero Morogoro, Stella Fabian  Masulya (42) Ukerewe Mwanza,  Regina Kapili Stephano (19)  Mpanda  Katavi, Rehema Daniel  Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.

WEKEZA KWA WAKULIMA WANAWAKE WADOGO WADOGO INALIPA 
 

No comments: