Mshiriki
wa Mafunzo ya utekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa
habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini akichangia
wakati wa mafunzo hayo kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Makiba,
wilayani Arumeru mkoani Arusha, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu kupitia mradi huo , Tarehe 13 Juni, 2015.
Mratibu
mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya
tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya
utekelezaji wa mradi huo kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, tarehe 13 Juni,
2015, wengine ni wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Washiriki
kutoka kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiwa katika picha ya
pamoja na Mratibu mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa
na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel (wa kwanza kushoto) mara
baada ya kufunga mafunzo ya utekelezaji wa mradi huo, tarehe 13 Juni, 2015.
Washiriki
kutoka kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiwa katika picha ya
pamoja na Mratibu mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa
na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel (wa kwanza kushoto) mara
baada ya kufunga mafunzo ya utekelezaji wa mradi huo, tarehe 13 Juni, 201
Serikali za vijiji zatakiwa kuhusisha Maafa ya mabadiliko ya
tabianchi na mipango ya maendeleo.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa kupitia mradi wa
kuimarisha mifumo ya habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari
nchini imezitaka serikali za mitaa na vijiji nchini kuhusisha maafa
yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi na mipango yao ya maendeleo, ili
kuhakikisha jamii inakuwa na uchumi bora na uwezo wa kupunguza athari za
maafa hayo.
Akiongea wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya
Maafa wa kata ya Makiba Wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Mratibu Mradi
huo Kitaifa, Alfei Daniel tarehe 13 Juni, 2015, alisema serikali za
vijiji zitumie taarifa za athari za mabadiliko ya tabianchi za vijiji
vyao ambazo zitakuwa zinaainishwa kupitia mradi huo kama sehemu ya
kuandaa mipango mikakati ya maendeleo vijijini.
“Kupitia mradi huu tutakuwa tunatoa taarifa za hali ya hewa kwa eneo
husika na kwa wakati, Ufahamu juu ya Hali ya hewa, mabadiliko ya
tabianchi, maji na mazingira ni muhimu sana na ni kiungo kikubwa katika
kuandaa mikakati na mipango ya maendeleo vijijini, hii itasaidia
kuimarisha uwezo wa serikali za vijiji kuwalinda wananchi kwa athari
zinazoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabianchi” alisisitiza Daniel.
Aliongeza kuwa uwepo wa miundombinu hafifu vijijini, upungufu wa
wataalamu wa masuala ya hali ya hewa pamoja na taarifa za hali ya hewa
kutowafikia wanavijiji kwa wakati, kumekuwepo na matumizi madogo ya
taarifa za hali ya hewa kitendo ambacho huziweka jamii za vijijini
katika mazingira magumu hasa kwenye shughuli za kiuchumi pindi
yanapotokea maafa ya mabadiliko ya tabianchi kama ukame na mafuriko.
Akiogea wakati wa mafunzo hayo Diwani wa Kata ya Makiba, Wilayani
Arumeru Mkoani Arusha, Mwanaidi Kim alifafanua kuwa ni muhimu vijiji
kuhusisha maafa yatokanayo na maafa ya mabadiliko ya tabianchi katika
mipango ya maendeleo kwani athari zake zinapotokea shughuli za maendeleo
hukwama.
“Katika kata yangu kuna vijiji sita ambavyo ni; Makiba, Patanumbe,
Valesika, Engatani na Kaloleni, lakini katika vijiji hivi vyote kuna
ishara ya upungufu wa chakula, Hivyo kama mtu hana chakula ni vigumu
kufanya shughuli za maendeleo lakini kupitia mradi huu athari hizi
hazitatupata tena kwani tutakuwa tunapata taarifa za hali ya hewa kwa
wakati na sisi tunapanga vizuri mipango yetu ya kimaendeleo” alisema
Mradi huo ambao utatekelezwa nchi nzima, kwa sasa unatekelezwa kwa
majaribio tangu mwaka 2014 hadi 2018 katika Halmashauri ya wilaya ya
Meru, Mkoani Arusha na Halmashauri ya wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment