Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia harakati za matengenezo ya Vitabu vya Baketi katika Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi wakati alipofanya ziara fupi ya Kutembelea kiwanda hicho.Kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bibi Hanat mohammed Aboud.
Mkuu wa Kitengo cha Kompyuta katika Kiwanda cha uchapaji Maruhubi Nd. Moh’d Abass Rajab akimuonyesha Balozi Seif aina za michoro tofauti inayosarifiwa katika uchapaji wa vitabu na majarida mbali mbali yanayopelekwa na wateja kuchapishwa kwenye kiwanda hicho.
Mfanyakazi wa Kitengo cha Kompyuta Bibi Miza Mkiwa Jecha akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Sampuli za picha na majarida yanayotengenezwa na mashine za kisasa za Kiwanda hicho.
Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Kaimu Mkurugenzi za Uchapaji Bibi Hanat Mohammed na Kushoto ya Balozi Seif n Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Na Mwandishi wetu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeonya kwamba haitamvumilia mtendaji ye yote wa Serikali au Taasisi zake za Umma atakayebainika anazorotesha ufanisi wa kazi pamoja na kuendeleza makundi katika sehemu za kazi.
Onyo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Idara ya upigaji chapa na Mpiga chapa Mkuu wa Serikali baada ya kuangalia utendaji kazi wa fanyakazi hao katika sehemu mbali mbali za Kiwandi hicho hapo Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema yapo mambo yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi za Umma ambayo hayapendezi kwa vile yanazorotesha ufanisi wa kazi kutokana na baadhi yao kupenda majungu na uvivu wa uwajibikaji.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba wapo watendaji katika Kiwanda cha Uchapaji wenye tabia ya kuendeleza uvivu jambao ambalo linawavunja moyo wenzao walioamua kufanyakazi kwa juhudi. Hivyo watendaji hao wanapaswa kujirekebisha mara moja.
Alifahamisha kwamba tabia hiyo mbaya inaiumiza Serikali Kuu iliyoamua kutumia fedha nyingi za kigeni katika kuimarisha miundo mbinu ya kisasa ya Kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha katika kiwango chaTeknolojia ya kisasa.
“ Pamoja na changamoto zinazokukabilini katika utendaji wenu wa kazi lakini Serikali kamwe haitosita kumchukulia hatua mtendaji ye yote atakayeonyesha tabia ya kuanzisha makundi na uvivu katika kazi “. Alisema Balozi Seif.
Aliwaeleza wafanyakazi hao wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali waelewe kwamba wanawajibika katika eneo muhimu kwa Taifa jambo ambalo wanahitajika kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifafanua kwamba Ofisi yake inayosimamia Kiwanda hicho iko katika matayarisho ya kuandaa Rasimu itakayoiomba Serikali Kuu kukifanya kiwanda hicho mabadiliko ya kuwa Mamlaka inayojitegemea.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuiongezea mapato Taasisi hiyo yatakayokidhi huduma za uendeshaji kamili pamoja na mafao ya wafanyakazi waoenbdesha Kiwanda hicho.
Mapema Wafanyakazi hao walielezea changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ambazo zimekuwa zikichangia kupunguza ari yao ya kjazi.
Walisema tatizo la usafiri kwa watendaji wanaomaliza kazi nyakati za usiku limekuwa mtihani mkubwa wa muda mrefu, posho kwa muda wa ziada pamoja na ukosefu wa mafunzo kweza kuzimudu vyema mashine za kisasa wanazotumia.
Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya changamoto hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed alisema kwamba Wizara hiyo itaomba ruhusa ya Serikali Kuu kununua Gari itakayosaidia kupunguza changamoto ya usafiri kwa watendaji hao.
Dr. Khalid alisema tatizo la posho za ziada kwa watendaji hao zimekuwa zikilipwa na Wizara kwa mujibu wa maombi yhanavyopelekwa licha ya kwamba Taasisi hiyo imekuwa ikitumia fedha za ziada za Idara nyengine katika kununulia mali ghafi za kuchapisha kazi muhimu za Taasisi za Serikali.
Akigusia suala la mafunzo Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa Wizara ina mpango wa kuwapeleka mafunzoni wafanyakazi watano wa Kiwanda hicho kwenye kwenye mashine zinazofanana na zile wanazotumia ili wapate uzoefu.
No comments:
Post a Comment