Friday, June 12, 2015

COCONUT FM ZANZIBAR WAANDAA BONANZA LA "PEPEA"

KITUO CHA RADIO CHA COCONUT FM ZANZIBAR CHAANDAA BONANZA LA "PEPEA" KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA, KATIKA VIWANJA VYA MAISARA MJINI UNGUJA TAREHE 16 JUNE, 2015. 

Kituo Cha Radio Cha Coconut FM Kilichopo Zanzibar Kwa Kushirikiana na Idara ya Wanawake na Watoto, Kimeandaa Bonanza linaloitwa "PEPEA - Uhuru Wa Nafsi, Akili na Mwili" litakalozinduliwa Jumanne tarehe 16 June, 2015 SIKU YA MTOTO WA AFRIKA katika Viwanja vya Maisara mjini Unguja kuanzia saa 8 Mchana.

Bonanza hili lenye lengo la kuhamasisha Wananchi juu ya Kulinda na Kutetea Haki za Watoto Zanzibar, linatarajiwa kuhudhuriwa na Wadau Mbalimbali wa Haki za Mtoto, Watoto wa Mabaraza ya Watoto, Wazazi, Walezi, Walimu, Wanafunzi, Wanasheria, Wanahabari na Viongozi wa Dini, Kuunganisha nguvu pamoja katika Kupinga na Kupiga Vita Vitendo vya Udhalilishaji dhidi ya watoto, Ukiukwaji wa Haki za Watoto pamoja na "Kutokomeza Ndoa za Utotoni na Mimba za Umri Mdogo".

Burudani za Kupambia Tamasha ni IGIZO kutoka kwa Watoto wa Mabaraza, Jakaya, Ras Ndaroh, Wakata Minazi Comedy pamoja na Ngoma ya Kilua.

PEPEA Bonanza litakuwa likifanyika Mara mbili kwa Mwaka, Tarehe 16 June (Siku Ya Mtoto Wa Afrika) kila mwaka na Tarehe 20 Novemba (Siku Ya Watoto Duniani) Kila mwaka.

PEPEA Bonanza 2015, limefadhiliwa na MRADI WA  KILIMO BIASHARA (MIVARF), mradi wenye lengo la kuwaunganisha wakulima na masoko na taasisi za fedha, kwa Kushirikiana na Coconut Media Group, Kituo Cha Huduma Za Sheria Zanzibar (ZLSC), Cool Coco Accessories, Diligent Consulting Ltd, Save The Children, ZIFF pamoja na Nyumbani Kwanza Media.

No comments: