Benki ya NMB imeidhinisha shilingi Bilioni 52 kama gawio kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwa mwaka 2014.Gawio hilo ni sawa na Shilingi 104 kwa kila hisa moja na ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka gawio la mwaka jana.
Gawio hilo ni kutokana na faida ya shilingi Bilioni 156 baada ya kodi iliyopatikana kwa mwaka 2014. Faida hiyo na gawio lililoidhinishwa ni Faraja kwa wanahisa wanaojivunia benki bora yenya matawi mengi kuliko benki yoyote Tanzania ikiwa na matawi zaidi ya matawi 163 na ATM zaidi ya 550 huku huduma zake zikiwa zimeenea kila wilaya hapa nchini.
Gawio hilo liliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi na kupitishwa na wanahisa katika mkutano mkuu wa Mwaka wa wanahisa uliofanyika siku ya jumamosi jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akiwasilisha mafanikio ya Benki ya NMB pamoja na Faida iliyoipata kwa mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa Mwaka wa wana hisa wa benki ya NMB iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, bodi ya wakurugenzi ya NMB ilipitisha gawio la Shilingi Bilioni 52 ikiwa ni gawio la shilingi 104 kwa kila hisa likiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka gawio la mwaka 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa NMB – Ineke Bussemaker akijibu hoja mbalimbali za wanahisa pamoja na kujitambulisha kwa wanahisa kama mkurugenzi mkuu mpya wa benki ya NMB katika mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika jumamosi jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, bodi ya wakurugenzi ya NMB ilipitisha gawio la Shilingi Bilioni 52 ikiwa ni gawio la shilingi 104 kwa kila hisa na likiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka gawio la mwaka 2013.
Maafisa Wakuuu kutoka vitengo mbalimbali vya NMB wakifuatilia mkutano wa wanahisa.
Mameneja wa kanda wa NMB kutoka kanda mbalimbali za benki ya NMB wakifuatilia Mkutano
Mkuu wa Wanahisa wa NMB.
Mkurugenzi mkuu wa NMB - Ineke Bussemarker akiongea na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi - Mike Laisser muda mchache kabla ya mkutano wa mwaka wa wanahisa wa NMB katika ukumbi wa Mwl Nyerere International Convention Centre.
No comments:
Post a Comment