Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015; (Picha na K-VIS MEDIA)
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya kujazwa na wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo Juni 8, 2015. Mheshimiwa Lowassa, amedhaminiwa na jumla ya wanachama 3,000 wilayuani hapo.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Losassa, akiwaaga wananchi na wana CCM waliofika kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Chato Juni 8, 2015.
Wakazi wa wilaya ya Geita, wakiwa juu ya mti ili kumuona aziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye ofisi za CCM wilayani Geita, Juni 8, 2015 kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
No comments:
Post a Comment