DAUDI YASSINI AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA KATIKA UWANJA WA WAMBI MJINI MAFINGA WAKATI WA FAINALI YA MASHINDANO YA MUUNGANO.
MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA AKIKAGUA TIMU KABLA YA MCHEZO
MGENI RASMI KATIKA FAINALI HIZO, MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA AKIWA KATIKA PICHA MOJA NA MABINGWA WA MUFINDI CUP TIMU YA MKOBA.
MGENI RASMI AKIWA KATIKA PICHA MOJA NA TIMU YA DODOMA ACADEMY
SEHEMU YA MASHABIKI WA WALIOJITOKEZA KATIKA MCHEZO HUO WA FAINALI
SEHEMU YA MASHABIKI WA WALIOJITOKEZA KATIKA MCHEZO HUO WA FAINALI
na fredy mgunda,iringa
mashindano ya muungano cup yafikia tamati hapo jana kwa mafanikio makubwa huku timu ya mukoba ikishinda na kuwa bingwa mpya kwa kumfunga timu ya dodoma academy goli mbili bila.
katika mchezo ulikuwa na mashabiki wengi katika uwanja wa wambi uliopo mafinga mjini na kuchezeshwa na marefa wenye weledi wa kazi yao na kuuchezesha mchezo kwa hali ya juu kiasi ambacho mashabiki walifurahia uwepo wa marefa hao katika mchezo huo.
mchezo huu ulikuwa wa vuta nikuvute kutokana na timu zote mbili kuwa katika kiwango bora katika mchezo huo hali iliyokuwa ikiwapa raha mashabiki kila muda kutokana na burudani ilikuwa ikitolewa uwanjani na wachezaji wa timu zote mbili.
kwa upande wake msimamizi wa mashindano hayo DAUDI YASINI alisema kuwa ni kazi ngumu sana kufanikisha mashindano hayo kutokana na kukosa wadhamini wa kudumu hivyo juhudi zake binafsi ndio zilizosababisha mashindano hayo kufanyika kwa mafanikio kipindi chote wakati akiwa msimamizi wa mashindano hayo.
baada ya mashindano hayo kumalizika katika uwanja wa wambi DAUDI YASINI alisimama mbeli ya maelfu ya mashabiki waliokuwa wamejitokeza na kuwaambia kuwa amejuudhuru rasmi kuendelea kusimamia mashindano hayo ambayo amekuwa akisimamia kwa miaka kadha iliyopita.
DAUDI YASSINI aliwapondeza wadau mbalimbali waliokuwa wakimuunga mkono katika harakati zote za kuandana mashindano hayo na kuwaomba waendelee kuwaunga mkono wasimamizi wengine watakao kuwa wakisimamia hapo baadae.
No comments:
Post a Comment