Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya
Tanzania (wa kwanza kushoto), Bw. Waleed Malik, Mwakilishi kutoka Benki ya
Dunia (wa pili kushoto), Bi. Neema Ndunguru, Mkurugenzi wa Mazingira ya
Biashara (PDB) pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia wakiwa meza kuu
wakati wa Kikao cha majadiliano katika ya Mahakama na Wadau wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara kupata maoni juu ya maboresho ya huduma za Mahakama. (IMG.
7436)
Mmoja wa wadau walioshiriki katika warsha hiyo akitoa
maoni yake katika majadiliano hayo. (IMG. 7449)
Washiriki wakiwa katika kazi za makundi wakitoa maoni
juu ya Mpango Mkakati wa Mahakama wenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma
zake. (IMG. 7465) (Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Na Mary Gwera
KATIKA mwendelezo wa maboresho ya utoaji wa huduma ya haki nchini,
Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kukutana na wadau pamoja na Washirika mbalimbali wa maendeleo ili kupata maoni
yao juu ya uboreshaji wa huduma zake.
Akiongea na Waandishi wa Habari mapema jana, katika Warsha iliyoandaliwa
na Mahakama ikishirikisha Ugeni kutoka
Benki ya Dunia na Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka, TRA,
Umoja wa Taasisi za Kifedha,MOAT, TIRA, TCRA n.k iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli
ya Hyatt jijini Dar es Salaam, Bw. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania alisema Mahakama imekuwa katika mchakato wa maboresho na washirika
mbalimbali wa Maendeleo na wadau wa utoaji haki ili kuboresha huduma zake.
“Mikakati hiyo ya maboresho ni sehemu ya mpango wa miaka mitano (5) ya
maboresho ya Mahakama ambapo unaenda sambasamba na maboresho ya miundombinu ya
majengo ya Mahakama, matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nk”
Alisema Kattanga
Mtendaji alisema maoni yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali wa
Mahakama utasaidia kubadili mtazamo mbaya wa wananchi walionayo kuhusiana na
Mahakama na hivyo kusaidia kujitathmini na kubadili mfumo wake wa utoaji wa
huduma.
Aliongeza kuwa maboresho hayo yataenda sambasamba na kubadili mfumo wa
ushughulikiaji wa malalamiko kuhusiana na mashauri mbalimbali na kurahisisha
taratibu mbalimbali za kisheria zitakazowezesha wananchi kupata urahisi katika
ufunguaji wa mashauri.
Kwa upande wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu-Ethiopia, Mhe. Dkt.
Menbere Tseha Tadesse, ambaye ni miongoni wa Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia
(World Bank), alisema kasi ya jitihada mbalimbali zilizowekwa na Mahakama ya
Tanzania katika kuboresha huduma zake inatia moyo.
Alisema ufanisi wa Mpango Mkakati wa Mahakama utategemea maoni ya wadau
mbalimbali wa Mahakama ili kupata njia bora za kuboresha huduma zake kwa
wananchi.
Naye, Bw. Henry Mwanyika, Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari
(MOAT), alisema amefurahishwa na uamuzi uliofanywa na Mahakama wa kujitathmini
utendaji wake ambao umekuwa shirikishi, akiongeza kuwa uamuzi huu utawezesha
Mahakama kupata maoni ya wadau ya nini kifanyike katika kuboresha huduma zake
kwa wananchi.
“Kwa kweli nimefurahishwa sana na uamuzi wa Mahakama wa kutushirikisha
sisi wadau katika mpango wake wa maboresho na tunahaidi kushirikiana nao bega
kwa bega katika jitihada hizo,” alieleza.
No comments:
Post a Comment