Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Kagera, Fikira Kisimba (katikati)
akifuatilia mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa
waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015, (mwenye miwani) ni
Mkurugenzi msaidizi (Mipango na Utafiti), Idara ya Uratibu maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho.
Mwakilishi wa Mkuu wa Polisi wilaya ya Bukoba, Mkaguzi John Kayunga
akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa katika Jeshi la Polisi
mkoani Kagera wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu
maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa katika Jeshi la Polisi
mkoani Kagera wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu
maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
Mratibu maafa wilayani Muleba Mkoani Kagera, Ruth Ishabakaki
akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa wilayani Muleba wakati wa
mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu maafa mkoani Kagera
tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu
maafa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Baadhi ya waratibu Maafa mkoani Kagera wakifuatilia mafunzo ya
menejimenti ya maafa kwa waratibu hao tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo
hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
menejimenti ya maafa kwa waratibu hao tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo
hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Mratibu Maafa, Idara ya uratibu maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Benedict
Kisaka akitoa mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa
waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
Kisaka akitoa mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa
waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
Na. Mwandishi
Maalum
Kamati za kuratibu maafa katika ngazi ya
serikali za mitaa zimetakiwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ya menejimenti
ya maafa ili kuweza kujenga jamii yenye uwezo wa kuzuia na kukabili maafa
yanayotokea katika maeneo yao.
Akifungua mafunzo ya waratibu wa maafa mkoani Kagera, tarehe 24
Juni, 2015, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa
huo, Fikira Kisimba alieleza kuwa nguvu ya uwezo wa jamii kuweza kukabili maafa itapatikana
iwapo kamati za kuratibu maafa katika ngazi za serikali za mitaa zitawajibika
wakati wote kwa kutokuwa zinasubiri uratibu wa maafa yanapotokea .
“Tunazo kamati za maafa kuanzia ngazi za
vijiji , vitongoji, kata , wilayani hadi mkoani lakini kamati hizi zinasikika sana
wakati maafa yanapotokea hali ambayo si nzuri katika hatua za menejimenti ya
maafa, kwani tunaposema menejimenti ya maafa tunazingatia, kuzuia,
kukabili maafa na kurejesha hali ya
awali baada ya maafa kutokea” alisema Kisimba.
Kisimba aliongeza kuwa mkoa wa Kagera
umekuwa ukikumbwa na maafa ya upepo mkali ambapo alibainisha kuwa wilaya ya
Muleba imewahi kupatwa na maafa hayo pamoja na maafa ya Kimbunga katika kisiwa
cha Goziba lakini wilayani Misenyi magonjwa ya mlipuko yamekuwa yakijitokeza
hivyo kamati husika zikiwajibika athari za maafa haya zinapunguzika.
Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkurugenzi
msaidizi (Mipango na Utafiti), Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Naima Mrisho alizitaka kamati za serikali za
mitaa na vijiji mkoani humo
kuhusisha maafa na mipango yao ya maendeleo, ili kuhakikisha jamii inakuwa na
uwezo wa kupunguza athari za maafa hayo.
“Ili kamati za maafa ziweze kuwajibika ipasavyo
hatunabudi Mipango ya maendeleo katika serikali za mitaa ihusishe maafa ili
jamii iwe na uwezo wa kukabiliana na maafa wakati janga linapotokea na wakati
wa kurejesha hali. Kamati za ” alisisitiza Mrisho.
Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Idara
ya Uratibu Maafa itaendelea kutoa elimu na kushirikisha Wadau ili
kuimarisha uwezo wa nchi katika kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza na
kukabiliana na athari za maafa yanapotokea.
No comments:
Post a Comment