Thursday, June 11, 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAIFA LA SWEDEN

Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye kilemba).
 Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchiniambaye pia ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani)Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha Hemela akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Mulamula akiendelea na hotuba yake,kushoto ni Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe.Lennarth 
 Balozi Lennarth  na Katibu Mkuu Balozi Mulamula pamoja na wageni waalikwa wakinyanyua glasi kutakiana kheri katika ushirikiano wa nchi hizi mbili.
 Balozi wa Sweden Mhe.Lennarth  akicheza kwa furaha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo hapa nchini kama ishara ya kufurahia maadhimisho ya siku ya Taifa lao la Sweden sherehe zilizofanyika katika makazi ya balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha watoto wa Maafisa wa Ubalozi wa Sweden hapa nchini walioshiriki hafla hiyo kwa wakiimba kwa ufasaha nyimbo za Mataifa ya Sweden na Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa   Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na     Waandishi wa abari katika hafla hiyo.Picha na Reuben Mchome.

No comments: