Thursday, June 18, 2015

AIRTEL YAZINDUA MICHUANO YA ARS 2015

 Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
michezo Leonard Thadeo akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa
Airtel Rising Star msimu wa tano. Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini
Dar es Salaam leo 17th June,2015.
 Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
michezo Leonard Thadeo akiwa alama ya uzinduzi wa kampeni ya " Its
Now" yenye kuwawezesha vijana  kutimiza ndoto zao katika Nyanja
mbalimbali kama technologia, michezo na muziki. Wakishuhudia ni Rais
wa TFF Jamali Malinzi( kushoto) Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi
Beatrice Singano Malya (kulia) akifatiwa na mwenyekiti wa soka la
vijana Bwana Ayoub Nyenzi
 Wachezaji wa Airtel Rising Star 2013 ambao sasa wanachezea timu ya
wanawake ya Taifa Twiga Stars wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
uzinduzi wa program ya Airtel Rising Stars ya msimu wa 5 iliyofanyika
katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania
 Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
michezo Leonard Thadeo (katikati) pamoja na Rais wa TFF Jamali
Malinzi( kushoto) Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice
Singano Malya (katikati kulia) akifatiwa na mwenyekiti wa soka la
vijana Bwana Ayoub Nyenzi
 Rais wa TFF Jamali Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa program ya
Airtel Rising Stars msimu wa tano program yenye lengo la kuinua na
kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya miaka 17.
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya akiongea wakati wa uzinduzi wa program ya Airtel Rising Stars msimu wa tano program yenye lengo la kuinua na kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya miaka 17.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa tano wa mashindano ya
soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo yataanza kutimua vumbi Agosti 8 katika ngazi ya awali na kuhitimishwa kwa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 - 21 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano amesema kampuni ya Airtel Tanzania  ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka minne iliyopita.

"Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua
vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu
za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20", alisema Singano.

Kumbukumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake
imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo
madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Singano pia ametangaza kampuni ya Airtel kuingia mkataba na nahodha wa 
Ivory Coast na kiungo wa Manchester City Yaya Toure katika kampeni
mpya iitwayo  "It's Now" yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani
Afrika kupitia Nyanja mbalimbali kama vile michezo, ikijumuisha
mashindano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya umri wa miaka
17.

Sehemu nyingine ambazo kampeni hii itazigusa ni mtindo wa maisha na
muziki, ambapo wateja watapata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya
kiteknolojia ili kuona fursa zinazowazunguka.

Huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa michuano ya Airtel Rising Stars
kufanyika hapa nchini Tanzania ambayo huanzia ngazi ya chini hadi
Taifa. Singano alilipongeza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania
(TFF) pamoja na serikali kupitia Wizara ya Michezo kwa kuiunga mkono
kwa dhati michuano ya Airtel Rising Stars tangu ilipoanzishwa nchini
mwaka 2011.

Mkurugenzi wa Idara ya michezo katika wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo ambaye alikuwa mgeni rasmi,
alisema serikali inatambua mchango wa Airtel katika kuibua vipaji vya
wanasoka chipukizi.

 "Inatuwia vigumu kuwekeza kikamilifu katika
michezo kwa sababu ya kulemewa na majukumu mengine muhimu ya kijamii 
ndio maana tunahamasisha sekata binafsi kujitokeza kusaidia na Airtel 
wanafanya kazi nzuri" alisema Thadeo.

Mwaka huu michuano ya ARS itajumuisha mikoa ya Ilala, Kinondoni,Temeke 
Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana na huku upande wa 
wasichana ukiwakilishwa na mikoa ya Ilala,Kinondoni, Temeke, Mbeya na 
Arusha.

Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliipongeza Airtel Tanzania
kwa kuwekeza kwenye soka la vijana. "Nawapongeza sana kampuni ya
Airtel Tanzania kwa mpango wake huu wa kuwekeza kwenye soka la vijana
ambao kwa kweli ndio msingi wa maendeleo wa mpira wa miguu hapa
Tanzania na duniani kote", alisema.

Airtel ni kampuni ya simu za mkononi yenye matawi barani Afrika katika
nchi za Burkina Fasso, Chad, Congo, Brazzaville, DRC, Gabon, Ghana,
Kenye, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Selisheli,
Sierra-Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.

No comments: