Wednesday, May 13, 2015

MPANGO MKAKATI WA KULIPANGA JIJI LA MWANZA KWA MIAKA 25 IJAYO YA WAWADIA

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga akisoma taarifa ya ufunguzi wa mkutano wa kwanza kati ya minane inayotarajiwa kufanyika kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
SERIKALI imesema kutokana na Jiji la Mwanza kujengwa nyumba za kudumu bila mpangilio maalumu, imeanza mchakato wa kuainisha maeneo yote ya Wilaya ya Ilemela na Nyamagana yanayounda jiji hilo ili  sehemu makazi, biashara, viwanda na huduma za jamii zifahamike.

Imesema kabla ya kuanisha maeneo hayo, leo itaanza kukutana na  wadau wote na wananchi wa jiji hilo ili kupokea maoni na mapendekezo kabla ya kuanza utekelezwaji wa mpango huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa jana kwenye vyombo vya habari na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Faisal Issa,imesema  mpango huo umelenga kuondoa migogoro ya ardhi na uvamizi wa maeneo yasiyoruhisiwa.
Wadau wa mkutano kutoka idara za serikali, viongozi wa siasa, waandishi wa habari na wafanyakazi taasisi za umma.

Dk. Issa alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo katika mkutano wa kupokea maoni na kujadili jinsi ya kuainisha maeneo hayo na kuwataka wananchi kuhudhuria ili kujua sehemu wanapoishi pametengwa kwa ajili gani.

“Jiji la Mwanza lipo katika mchakato wa uandaaji mpango Kabambe ambao unazihusu wilaya ya Nyamagana na Ilemela ambazo kwa pamoja zinahusisha eneo la mipango ya  kilometa za mraba 437.
Wawekezaji.
Mchakato huu unahusisha pia kukutana na wadau mbalimbali ili kutoa fursa kwa mshauri wa mradi kuelekeza mukhtada wa uchambuzi kimkoa, maoni hayo ndiyo yatakayotoa uelekeo wa namna ya kulipanga jiji na kuondokana na ujenzi holela, hivyo mawazo ya wakazi husika yatazingatiwa.

“Mpango huu utaelekeza maendeleo ya mji wa Mwanza siku za usoni kwa kuzingatia kuwa Mwanza ni mkoa uliojaaliwa  kuwa na mandhari yenye maua, miti, mimea na madini mbalimbali, pia  Mwanza ni nguzo ya viwanda Tanzania na kitovu muhimu  cha biashara kanda ya Ziwa Victoria,”alisema Dk. Issa.

Hata hivyo alisema, katika mkutano wa leo, watalaamu, wabunge na viongozi mbalimbali wa Serikali wa wizara zote wanatarajiwa kuhudhuria kwa kuwa mpango huo unagusa kila sekta.

Alisema baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa sekta zote, wananchi watajulishwa kila hatua ili kujua mipango ya Jiji la Mwanza litakavyokuwa hapo baadaye.
Wanasiasa, jeshi la polisi, viongozi wa dini na wadau mbalimbali mkoani Mwanza.
Wataalamu wa michoro na ramani.
Madhumuni na Malengo
Picha ya Meza kuu na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa.
Sekta.
Picha ya pamoja meza kuu na Jeshi la polisi Mwanza.
Picha ya pamoja waandishi wa habari na meza kuu.
Meza kuu na wataalamu wa sekta mbalimbali mkoani Mwanza.
Sekretarieti.
 PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA.

No comments: