Wednesday, May 13, 2015

KIWANDA CHA PAMBA AMBACHO PAMBA YAKE ILITEKETEA KWA MOTO MKOANI SHINYANGA CHAPATA BIMA YAKE TOKA UAP

Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Bima ya UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto) wakitenbelea kiwanda hicho kujionea shughuli za utendaji ikiwa ni pamoja na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho mara baada ya kukipatia bima ya shilingi milioni themanini (80,000,000/=)  kufuatia kuunguliwa na pamba yake katika ghala la kuhifadhia lililopo kiwandani hapo.
Mwanzoni mwa mwaka huu 2015 pamba iliyokuwa imehifadhiwa kwenye moja ya maghala katika kiwanda cha pamba JIELONG Holdings Tanzania LTD iliungua na kuharibika kabisha mara baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu hali iliyosababisha pamba hiyo kuchemka na kuwaka moto.
Ghalani.
Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto) akiwa na Meneja madai wa kampuni ya Bima ya UAP Bw. Michael Emmanuel .
Ili kuepuka udanganyifu toka kwa baadhi ya wateja wasio waaminifu wanaozusha majanga ili kunufaika na bima, kabla ya kulipa fidia ya bima kwa mteja Kampuni ya Bima ya UAP hufanya uchunguzi... ZAIDI BOFYA PLAY HAPA CHINI KUMSIKILIZA MENEJA MADAI.

Kampuni ya Bima ya UAP imeweka utaratibu wa kuwatembelea wateja wake kila msimu kwaajili ya kuona shughuli za utendaji na kutoa ushauri kwa wateja juu ya nyongeza mbalimbali za huduma zinazoongezeka. 
KAMPUNI ya Bima ya UAP iko mkoani Shinyanga kutembelea viwanda vya kusindika pamba, viwanda vya kutengeneza mafuta yanayotokana na mbegu za pamba na alizeti ikiwa ni pamoja na viwanda vya mashudu. 

UAP inawateja zaidi ya elfu arobaini nchini Tanzania. 

Sehemu ya majengo ya Kiwanda cha pamba cha JIELONG Holdings Tanzania LTD kilichopo mjini Shinyanga.
Nyuma ya majengo ya kiwanda.
Picha ya pamoja uongozi wa Kiwanda na maafisa wa UAP.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA

No comments: