Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Chato Mkoani Geita, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza
wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato wanaotarajiwa
kuhitimu masomo yao mwezi ujao.
Wanafunzi wa kidato
cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato Mkoani Geita wanaotarajiwa kuhitimu
masomo yao mwezi ujao wakiimba wimbo maalum wa Shule hiyo katika Mahafali ya 10
shuleni hapo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti mwanafunzi
mmojawapo katika mahafali hayo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya uchanaji wa
mbao katika Shule ya Sekondari Chato. Mbao hizo hutumika katika kazi mbalimbali
za ujenzi wa shule hiyo. Pia Dkt. Magufuli ameichangia shule hiyo kiasi cha
Shilingi Milioni tano.
Waziri Magufuli akikagua moja ya computer katika shule hiyo.kushoto
kwake ni Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mahendeka Mafele.
Dkt. Magufuli akipiga
ngoma pamoja na kikundi cha Skauti cha Shule ya Sekondari Chato kabla ya kuanza
kwa mahafali hayo.
Waziri wa Ujenzi
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua maabara ya shule hiyo.
Waziri Magufuli
akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chato Mwalimu Mahendeka
Mafele kuhusu Ujenzi wa vyoo unaoendelea.
Baadhi ya wazazi waliohudhuria katika mahafali
hayo ya kumi ya kidato cha Sita shuleni hapo.
Vijana wanaotarajiwa
kuhitimu kidato cha sita katika shule hiyo wakitoa burudani pamoja na Mwenyekiti
wa bodi ya Shule hiyo Bi Helena Busumilo.
Waziri Magufuli akifanya ukaguzi wa mabweni
shuleni hapo. P
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato
Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi bora wa Shule ya Sekondari Magufuli
Emanuel Sina Cheti cha Usafi na Utunzaji wa Mazingira kwenye mahafali ya nne ya
shule hiyo.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wanafunzi
pamoja na wazazi kwenye mahafali hayo ya nne katika Shule ya Sekondari Magufuli.
Wanafunzi wa kidato cha Sita katika shule ya
sekondari Magufuli wakifurahia hotuba
iliyokuwa ikitolewa na Mgeni rasmi Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
picha ya pamoja na wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao ya kidato cha
sita katika shule ya Sekondari ya Magufuli iliyopo Bwanga mkoani Geita.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Magufuli
wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za asili ya kisukuma katika mahafali
hayo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Magufuli Mwalimu
Abdalah Haji Siseme akimkabidhi risala mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato
Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua kambi ya mkandarasi anayejenga
barabara inayopita karibu na shule hiyo. Dkt. Magufuli ameiahidi shule hiyo
kuwa pindi mkandarasi atakapomaliza ujenzi wa barabara hiyo atakabidhi majengo
hayo kwa shule hiyo ya kidato cha tano na sita.
Mandhari ya shule ya Sekondari Magufuli. Shule
hiyo toka kuanzishwa kwake mwaka 2010 haijawahi kufelisha mwanafunzi hata mmoja.
DKT.
MAGUFULI AHIMIZA WAZAZI KUWASIMAMIA VIZURI WATOTO KATIKA ELIMU.
Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Chato mkoa wa Geita Dkt. John Pombe Magufuli amewahimiza wazazi na walezi
kuwasimamia vizuri watoto wao katika masuala ya elimu ili kuwaepusha na matendo
maovu katika jamii.
Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo leo katika
mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari ya Chato mkoani
Geita ambapo jumla ya wanafunzi 84 wanatarajiwa kuhitimu.
“Wazazi mnataikiwa kuhakikisha
mnawafatilia watoto wenu katika masomo yao na kuacha tabia ya kutoa uhuru
mkubwa ambao hutumika vibaya. Inabidi muwabane sana hata wakichukia leo kesho
watakuja kufurahi na kuona faida yake” alisisitiza Waziri Magufuli
Waziri Magufuli aliwaasa pia wanafunzi
wa kidato cha kwanza mpaka cha nne kuhakikisha kuwa wanasoma kwa bidii ili
waweze kufaulu kuingia kidato cha tano.
“Mnatakiwa kuanzia sasa kupanga mikakati mizuri ya kujisomea kwa muda huu
uliobaki na kwa mwaka huu kusiwe na daraja la nne katika matokeo yenu” aligusia
Waziri Magufuli
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari
Chato, Bi. Hellen Busumilo amewasisitiza wazazi kusaidiana na walimu katika
malezi ya watoto na pindi mtoto anapokosea aadhibiwe kwani kwa kutofanya hivo
ni kosa linalopelekea watoto kufanya matendo maovu.
“Usimamizi wa watoto ni jukumu la wazazi
wote, mzazi nyumbani na mwalimu shuleni
ili tuweze kuwasaidia watoto wetu hasa watoto wa kike” alisema Bi Busumilo
Bi. Busumilo aliongeza kuwa kuna haja
ya kuwaelimisha na kuwafundisha watoto mambo mbalimbali yatakayowajega kwasasa
na badae.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Chato, Mwalimu Mafere Mahendeka amemshukuru Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kuhudhuria mahafali hayo ya 10 ya kidato cha Sita katika shule
hiyo.
“Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri
kwa michango yako mbalimbali katika shule yetu, mfano mwaka 1997 ulisaidia shule hii kumilikiwa na
Serikali kwa manufaa ya umma, na kwa mwaka 2003 ulifanikiwa kuweka kidato cha
tano na sita”, Alisema Mwalimu Mafere.
Mwalimu Mafere amemhakikishia Waziri wa
Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. John Magufuli kuwa watatumia
kiasi cha Shilingi milioni tano alizowapa katika mahafali hayo kwa ajili ya
maendeleo ya Shule hiyo na si vinginevyo.
Shule ya Sekondari ya Chato ina jumla
ya wanafunzi 1018 kuanzia kidato cha I-VI. Shule hii imekuwa ikifanya vizuri
katika mitihani ya kitaifa kidato cha sita, mfano mwaka 2011 ufaulu ulikuwa
asilimia 96 na mwaka 2014 ufaulu ulikuwa asilimia 100.
Wakati huo huo, Dkt. Magufuli ameahidi kuwa majengo ya kambi ya
mkandarasi katika barabara ya Bwanga-Uyovu yatakabidhiwa kwa shule ya sekondari
Magufuli pindi kazi za ujenzi wa barabara hiyo utakapokamilika.
Ahadi hiyo ilitolewa na Waziri Magufuli
katika mahafali ya nne ya kidato cha sita katika shule ya
Sekondari Magufuli ambapo jumla ya wanafunzi 48 wanatarajiwa kuhitimu masomo
yao mwezi ujao.
“Sitafurahi kuona wanafunzi wakipata
tabu na walimu wakishindwa kufanya kazi zao vizuri kwa kukosa nyumba za kuishi
na madarasa ya kufundishia hivyo huyu mkandarasi akikamilisha kazi za ujenzi wa
barabara, hizi nyumba 12 zinabaki kuwa mali yenu”, alisema Dkt. Magufuli.
Aidha, Waziri Magufuli aliwasihi
wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuacha kufikiria changamoto zilizopo shuleni
hapo kwasababu wenzao waliowatangulia walifanya vizuri licha ya changamoto hizo
“Pamoja na changamoto zilizopo
mnatakiwa msome kwa bidii na muache mambo mengine kwanza ili ikiwezekana wote
hapa mfaulu kuingia chuo kikuu na kuendelea kuiletea sifa shule yenu na Wilaya
kwa ujumla”, alisisitiza Waziri Magufuli
Kuhusu suala la umeme ambalo pia ni
changamoto shuleni hapo, Dkt. Magufuli amewataka kuwa na subira kwani tayari
suala hilo lipo katika mpango wa Umeme vijiji REA ambapo umeme utafika katika
tarafa hiyo ya Bwanga hadi eneo la shule ili kupunguza adha wanayoipata wanafunzi
hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Chato, Rodrick Mpogolo amesema kuwa tarafa ya Bwanga ina watoto 81 ambao mpaka
sasa hawajaripoti kwenye shule za Sekondari na ametoa hadi tarehe 13 mwezi huu watoto
wote wawe wameripoti shuleni hata kama hawana sare za shule.
“ili kupata wanafunzi wa kuingia kidato
cha tano hatuna budi kuwekeza kwenye elimu ya Sekondari hivyo basi nawasihi
sana wazazi mpaka muda huo uliopangwa muwe mmewapeleka watoto shuleni baada ya
hapo ni msako utafanyika ili wazazi watakao goma tuwachukulie hatua kali za
kisheria.”, alisisitiza Mkuu wa Wilaya ya Chato.
Shule
ya Sekondari Magufuli ilizinduliwa tarehe 21/10/2009 na aliyekuwa Waziri wa
Elimu katika kipindi hicho Profesa Jumanne Maghembe. Shule hiyo ina jumla ya
wanafunzi 140 wa kidato cha tano na cha Sita na imekuwa ikifanya vizuri kati ya
shule zenye wanafunzi zaidi ya 30 katika ngazi za Wilaya, Mkoa na Kitaifa.
No comments:
Post a Comment