Wednesday, April 15, 2015

Airtel yakabithi magari kwa washindi 8 wa Mkoa wa Dar es saalam

 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Lilian Festo Mjimba katika hafla iliyofanyika Makao
Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa droo hiyo.
  Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Lilian Festo Mjimba katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
  Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Mama lishe Efgenia Mathew Mushi katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa droo hiyo.
 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Kinyozi Juma Ally Songoro katika hafla iliyofanyika
Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. 
 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Kinyozi Juma Ally Songoro katika hafla iliyofanyika
Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za magari mapya aina ya Toyota IST, kwa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, (kutoka kushoto), Subeti Salim Subeti, Kuruthumu Seleman Forogo, Juma Ally Songoro, Liliani Festo Mjimba, Christone Edick Mbalamula, Efgenia Mathew Mushi na Obel Samwel Mwamugiga katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
 Mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Subeti Salim Subeti akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), funguo ya gari jipya aina ya Toyota IST, baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania,
Frank Filman (kushoto), katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni watoto wa mshindi huyo.
Mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Kuruthumu Seleman Forogo akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), funguo ya gari jipya aina ya Toyota IST, baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel
Tanzania, Frank Filman (kushoto), katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia ni kaka wa mshindi huyo, Yasin Juma.

Airtel yakabithi magari kwa washindi 8 wa Mkoa wa Dar es saalam
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabithi magari kwa
washindi wake waliokuwa wamesalima kwa mkoa wa Dar es saalamu
walioibuka washindi katika droo za mwisho za promosheni ya Airtel
yatosha zaidi.

Washindi waliokabithiwa magari yao ni pamoja na  kuruthumu Seleman
(42) mfanyabishara ndogondogo, Lilian Mgimba (24) mfanyabishara
ndogondogo, Christ Mbalamula (27) mjasiliamali , Juma Songoro(24)
Mwanafunzi wa chuo cha IFM , Subeti Salum Subeti (43) kondactor wa
daladala, Isgnenia Mushi(35) mfanyabishara ndogondogo,Charles Msakwa
(45) Mwalimu, na  Obed Muamugija (24) Mwanafunzi wa chuo cha IFM.

Akiongea wakati wa kukabithi magari hayo Mkurugenzi wa kitengo cha
teknolojia habari wa Airtel Bw, Frank Filman alisema “ nawashukuru
sana wateja wetu kwa kutumia huduma zetu hususani huduma ya Airtel
yatosha zaidi ambayo mbali na kuwazawadia wateja wanaotumia vifurushi
kupitia promosheni ya Airtle Yatosha zaidi tumewawezesha wateja wetu
kupata huduma bora, za nafuu zinazokithi mahitaji yao ya kupiga simu,
kutuma ujumbe mfupi pamoja na huduma ya internet.

Leo tunajifuraha kukabithi magari kwa washindi 8 waliosalia katika
mkoa wa Dar es saalam, tunawaahidi washindi wengi waliosalia kutoka
kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa kuwa watakabithiwa magari yao
ndani ya wiki moja kuanzi sasa.

Tunawapongeza wateja Wetu wote waliobahatika kujishindia magari
kupitia promosheni hii tangu ianze na tunaamini tumeweza kuwawezesha
kufanya shughuli zao za kijamii na za kiuchumi kwa urahisi zaidi na
kuboreesha maisha yao na jamii ya Tanzania kwa ujumla

Tunawaahidi kuendelea kutoa huduma za mawasiliano bora, zenye ubunifu
huku tukiendelea kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuwazawadia
kupitia promosheni kama hii ya Airtel Yatosha Zaidi.

Promosheni ya Airtel yatosha imeshafikia mwisho wake lakini huduma
yetu ya Airtel yatosha bado inaendelea hivyo natoa wito kwa watanzania
kuendelea kujiunga na vifurushi hivi na kufurahia huduma bora zenye
gharama nafuu kwa wakati wote. aliongeza Filman.

Kwa upande wake moja ya washindi wa promosheni hii bi, Kuruthumu
Seleman alisema” mpaka sasa sijaamini kwamba nimeshinda gari, kwakweli
nawashukuru sana Airtel kwa kuanzisha promosheni hii. Kwakweli sikuwa
na wazo kama naweza kushinda, haya ni maajabu kwakeli kumbe kila
mtanzania anaweza kupata nafasi ya kushinda kupitia promosheni hizi za
Airtel.

Nafurahia ushindi huu kwa sasa kwani nilikuwa natamani kuwa na usafiri
na kupunguza adha nayoipata katika shughuli zangu za mama lishe, sasa
nauhakika wa kusafirisha chakula changu kwa usalama zaidi na kuwafikia
wateja wangu kwa wakati, naamini biashara yangu itaboreshwa na kukua
na kuwa ya ufanisi zaidi sasa kulinganisha na  ilivyokuwa awali”

Promosheni ya Airtel yatosha ilizindualiwa mwanzoni mwa mwezi wa
februari mwaka huu na kufika mwisho wake mwanzoni mwa mwezi Aprili
ambapo  jumla ya  wateja 60 wamejishindia na kukabithiwa magari yao
aina ya Toyota IST. Airtel iliwazawadia wateja wake gari aina ya
Toyota IST kila siku kwa muda wa siku 60

No comments: