WAHARIRI
22 wa Vyombo vya habari mbali mbali nchini jana walifanya ziara kwenye
Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) wakiongozwa na Jukwaa la
Wahariri Tanzania(TEF).
Katika
ziara hiyo Wahariri hao walipata maelezo mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa TBL,Roberto Jarrin kuhusu hali ya kibiashara ya kampuni hiyo pamoja
na bidhaa zinazozalishwa kisha kutembelea mitambo ya kutengeneza Bia.
Meneja
wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari aliwaambia Wahariri Changamoto
ambazo Kiwanda hicho kinakabiliana nazo kuwa ni pamoja na umeme wa grid ya
taifa kuwa na nguvu ndogo ya kutokutosha kuendesha mitambo, ubovu wa
barabara ya kuingilia kiwandani pamoja na upatikanaji wa maji.
Akitoa
Shukrani kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa TEF, Absolom Kubanda,
aliishukuru Kampuni ya TBL kwa kuwathamini na kuwaalika katika ziara hiyo
na kuongeza kuwa watakuwa mabalozi wazuri kutangaza hali halisi waliyoiona
kiwandani hapo tofauti na maneno ya watu mitaani.
Alisema
watu wengi hudhani mazingira ambayo vinywaji vinatengenezwa hayafai jambo
ambalo sio la kweli kutokana na kujionea wenyewe mlolongo mzima tangu
uoshaji wa chupa hadi kinywaji kinavyojazwa kuwa katika hali ya usafi.
Kwa
upande wake Meneja uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi alisema
lengo la kuwaalika Wahariri wa Vyombo vya habari ni kudumisha uhusiano
baina ya TBL na Vyombo vya habari.
Aliongeza
kuwa lengo lingine ni kutoa mrejesho kwa jamii juu ya hali ya kibiashara
ilivyosasa na awali kupitia kwa Wahariri wa Vyombo vya habari ili iwe wazi
kwa kila mtu.
|
|
|
Mkurugenzi
mkuu wa Kampuni ya Bia(TBL) na SUBMiller East Africa Operesheni,
Roberto Jarrin, akiwasilisha Mada kwa Wahariri wa Vyombo vya habari
nchini waliofanya ziara katika kiwanda cha Bia Tawi la Mbeya.
|
|
Meneja
wa Kiwanda cha Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akitoa maelezo kuhusu
kiwanda hicho kwa Wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini.
|
|
Meneja wa Kampuni ya Vinywaji ya Konyagi(TDL) akifafanua jambo kwa Wahariri wa vyombo vya habari.
|
|
Mkurugenzi
mkuu wa Kampuni ya Bia(TBL) na SUBMiller East Africa Operesheni,
Roberto Jarrin, akionesha kitu ubaoni kwa Wahariri wa Vyombo vya habari
nchini waliofanya ziara katika kiwanda cha Bia Tawi la Mbeya.
|
|
Steve Kilindo (Corporate affairs& legal director) akitoa maelezo kwa Wahariri.
|
|
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akibadilishana mawazo na mmoja wa watumishi wa TBL Mbeya. |
|
Wahariri wakifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa. |
|
Meneja Viwango wa TBL Esther Mmari akitoa maelezo juu ya viwango vya bia zinazozalishwa kwa Wahariri.
|
|
Baadhi
ya Watumishi wa TBL wakikagua makaratasi yaliyojazwa na Wahariri baada
ya kupewa kazi ya kuchagua Bia aina ya Kilimanjaro yenye ubora. |
|
Baadhi ya Wahariri wakiangalia kwa makini Bia zilizo kwenye grasi ili kugundua bia yenye ubora unaotakiwa.
|
|
Wahariri
pamoja na Watumishi wa TBL wakielekea kutembelea mitambo ya
kutengenezea vinywaji katika kiwanda cha Bia cha TBL tawi la Mbeya.
|
|
Meneja
wa Kiwanda cha Bia cha Mbeya Waziri Jemedari akitoa maelezo kwa
Wahariri wakiwa wanatembelea na kuangalia mitambo mbali mbali kiwandani
hapo.
|
|
Wahariri wakiwa Kiwandani wakiangalia mitambo mbali mbali. |
|
Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kutoka kwa Uongozi wa TBL.
|
No comments:
Post a Comment