Monday, March 16, 2015

TAASISI ZA SERIKALI, ASASI ZA KIRAIA ZAKABIDHIWA KATIBA ILIYOPENDEKEZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi  Tanzania (TPSF),  Godfrey Sembeye (kushoto), akipokea nakala ya Katiba inayopendekezwa kutoka kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, wakati wa hafla ya utoaji wa katiba hiyo kwa taasisi za serikali na asasi za kiraia iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande). 
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro akizungumza wakati wa kukabidhi Nakala za katiba iliyopendekezwa kwa taasisi za serikali na asasi za kiraia jijini Dar es Salaam.
 Nakala za katiba iliyopendekezwa.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania, Amon Mpanju (kushoto) akipokea nakala za Katiba iliyopendekezwa ambayo imeandikwa kwa maandishi ya nukta nundu kutoka kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro. Katikati ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania, Amon Mpanju (kushoto) akisoma moja ya nakala ya Katiba iliyopendekezwa iliyoandikwa kwa maandishi ya nukta nundu mara baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro kumkabidhi. Katikati ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu.

Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Ernest Kimaya akipokea nakala ya Katiba iliyopendekezwa ambayo imeandikwa kwa maandishi makubwa kutoka kwa Waziri wa Sheria na Katiba.
Mwakilishi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Said Mohamed Lenza akipokea nakala ya Katiba iliyopendekezwa.
Mwakilishi wa Bohora, Zainudin Adamjee akipokea nakala ya Katiba iliyopendekezwa.
Mwakilishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambaye ni Ofisa wa Sheria, Hussein Sengu akipokea nakala ya Katiba iliyopendekezwa.

No comments: