Sunday, March 15, 2015

uzinduzi cha chama NETEVE kinachojihusisha na mambo ya utamaduni wa Afrika nchini Ubelgiji

 Mheshimiwa Tim Vandenput Meya wa kitongoji cha Hoeilaart nchini Ubelgiji akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa chama cha NETEVE. Wa kwanza kushoto ni Rais wa chama hicho Madame Oliva Butoyi akishuhudia uzinduzi huo. Wengineo ni wanachama wanaounda umoja huo. Neteve ni chama kinachojihusisha na mambo ya tamaduni za nchi mbalimbali toka barani Africa.
Wanachama wa Neteve wakipiga makofi kushangilia uzinduzi rasmi wa umoja wao pale Mheshimiwa Tim Vandenput alipokata utepe kukizundua chama hicho rasmi.
Kikundi cha ngoma cha Amahoro kutoka Rwanda kikitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa chama cha Neteve nchini Ubelgiji 
Wasichana warembo wa Amahoro Music Dance wakifanya yao katika sherehe za uzinduzi wa chama cha Neteve[Picha na maelezo toka Maganga One Blog].
Wageni waalikwa toka mataifa mbalimbali wakiendelea kupata yanayojiri kwenye uzinduzi huo.
Rais wa chama cha Neteve akitoa hotuba ya kukitambulisha chama chao muda mfupi baada ya uzinduzi.[Picha na maelezo toka Maganga One Blog].
Afisa ubalozi wa Namibia kushoto pia alikuwa mgeni mwalika katika sherehe hizo wa uzinduzi
Wageni waalikwa wakiwa makini kusikiliza taratibu wilizokuwa zikiendelea
Waalikwa wakiendelea kusikiliza hotaba za viongozi mbalimbali hawapo pichani 
Microphone controler alikwa ni Dr Pendo
 Vijana wa Kitanzania wakiingia ukumbini kuonyesha mavazi asilia kutoka nyumbani Tanzania
 Mchungaji wa mwanamke toka nchini Maurituas akitoa hotuba fupi kabla ya kutoa burudani ya muziki wa katika ufunguzi wa sherehe za Neteve
 Katika sherehe za  ufunguzi wa umoja wa chama cha NETEVE kulikuwa na ngoma asilia ambazo zilikuwa zikipigwa na wazungu. 
 Burudani ya aina yake ilichukua nafasi katika sherehe za ufunguzi wa NETEVE
 Burudani ilikuwa nzuri na kila mmoja alishangilia kuona wazungu hawa wakicheza kwa ustadi mkubwa ngoma zenye asili ya kiafrika
Saitoti na nduguye wakifanya mambo yao kwenye sherehe za uzinduzi wa chama kisicho cha kiserikali cha NETEVE ambacho kinajishughulisha na mambo ya utamaduni
Mr na Mrs Saitoti
Mmoja wa wageni waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Neteve ni ndugu Saitoti kushoto akiwa na mkewe katikati na wa kulia kabisa ni mke wa Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji mama Kamala. Picha zote na maelezo toka Maganga One Blog. Jinsi ya kujua shughuli za chama hiki unaweza kujiunga na website yao hapa chini
http://www.neteve-asbl.com/index.php

No comments: