Mbunge wa Ludewa,Deo Filikunjombe akisisitiza jambo wakati akitoa salamu zake kwenye mazishi ya SR. Instrude maria
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Honolatus Mgaya kushoto na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kulia wakishirikiana na wananchi wa Njombe kubeba jeneza na SR. Maria.
Mbunge Filikunjombe katika usikivu mkubwa
Na Matukiodaima BLoG
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewaomba viongozi wa dini nchini
kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali wakiwemo wabunge ili
kuwatumikia wananchi kwa kutanguliza hofu ya Mungu ya kwatumikia wananchi waliowachagua
Kauli hiyo
aliitoa Jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtawa wa kanisa la
Romanikatoliki Parokia ya Imiliwaa Marehemu SR. Insetrud Maria
Alisema
kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kazi ya kuliombea Taifa na
watu wake ila wanasiasa na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwatumikia
wananchi kimwili hivyo kuna haja ya viongozi wa dini kuendelea kufanya
kazi ya kuwaombea viongozi .
" maandiko matakatifu yanasema
kuwa enendeni duniani mkawafanyi watu wote kuwa wanafunzi wangu...chama
cha walimu hapa wamesema kuwa SR.Maria alikuwa mwalimu mzuri hivyo ni
wazi alizifanya kazi zote ya kiroho na Kimwili "
Hivyo alisema
kwa kutambua mchango wake alioutoa hapa duniani Enzi za uhai wake kwa
upande wake ameguswa kujenga darasa katika shule ya sekondari parokioni
hapo Kama njia ya kumuenzi zaidi.
Filikunjombe alisema kuwa iwapo
kitajengwa kitu chochote cha kumbukumbu liwe darasa la shule ya msingi
ama sekondari ni kumbukumbu tosha .
Alisema mchango wa SR. Maria
katika maendeleo ya mkoa wa Njombe ni mkubwa na kuwa haitapendeza
mchango wake huo kuachwa bila kuenziwa.
" SR .Instrud Maria
mbali ya kazi yake ya utawa pia alikuwa ni mwalimu na mchango wake
katika shughuli zake ni mkubwa hivyo nawaombeni tumienzi kwa kujenga
darasa Moja ambalo litaandikwa jina lake Kama kumbukumbu ya sasa na
baadae" Kuwa kwa upande wake atahakikisha darasa hilo linajengwa kwa kupitia uwezo wake na wahisani mbali mbali .
SR.Maria alifariki juzi kwa ugonjwa wa shinikizo la Damu na mazishi yake kuongozwa na askofu wa jimbo la
Njombe Alfred Maluma .
walimu Njombe wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuweka shada
|
|
No comments:
Post a Comment