Monday, March 2, 2015

TANZIA: Mama wa Katibu wa Mbunge afariki Dunia, wilayani Kibaha mkoani pwani

MAMA wa Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum  Mhe. Al Shaimar Kweigyir, Bw. Semeni Kingaru, anayeitwa Kibibi Haji Pembe, amefariki Dunia leo saa tano asubuhi akiwa na umri wa miaka 80.
Semeni Kingaru kulia ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir, akiwa na mama yake mzazi Bi Kibibi Haji enzi za uhai wake. Marehemu Kibibi Haji  amefariki Dunia leo asubuhi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
Mama huyo amefariki nyumbani kwake kijiji cha Misugusugu,wilayani Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Bw. Kingaru amesema leo kuwa mama yake atazikwa kesho saa 10 jioni kijijini hapo.
Alisema kuwa kwa wataokwenda kwenye msiba huo watalazimika kushuka katika kituo cha kijiji cha Misugusugu ambapo ndipo sehemu atakapozikwa marehemu mama yake.
Msiba huo wakati unatokea, Bw. Kingaru alikuwa nchini Uganda katika majukumu yake na kulazimika kusitisha shughuli hizo kwa ajili ya kuwahi msiba wa mama yake.

No comments: