Monday, March 2, 2015

Elimu ya kidigitali ya Vodafone Foundation kuwanufaisha watoto 15,000 katika kambi za wakimbizi

Taasisi ya Vodafone Foundation leo imetangaza kuwa mpango wake wa kutoa elimu kidigitali umewezesha jamii zinazoishi kwenye mazingira magumu yanayosababishwa na majanga mbalimbali na  kujikuta zikiishi kwenye kambi za wakimbizi kuweza  kupata elimu.

Mpango huu wa   unatekelezwa katika  maeneo yenye mazingira magumu ambako kuna matatizo ya kutokuwepo nishati ya umeme na  upatikanaji wa mawasiliano hususani ya mtandao wa interneti na umeweza kutekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Ufunguzi wa madarasa chini ya mpango huu unafanyika kwa kutumia masanduku maalum yanayobeba vifaa vya kufundishia ,kuzalisha nishati ya umeme,kuchaji vifaa vya kufundishia na modemu maalumu za interneti ambazo hazihitaji kuunganishwa papo kwa papo .Vifaa vyote hivi vilivyoandaliwa kwa ajili ya mpango huu  unaoendeshwa kwenye maeneo yenye mazingira magumu vikiunganishwa kwa muda mfupi vinawezesha walimu maalumu walioandaliwa kuvitumia kuweza kuwapatia elimu wanafunzi bila matatizo yoyote.


Masanduku  maalumu ya kubeba vifaa vinavyotumika kutolea elimu hili yameandaliwa kutumika kuchaji vifaa vyote na vikishawekwa kwenye chaji kwa muda wa kati ya masaa 6-8 sanduku linaweza kutumika siku nzima kufundishia bila kuhitaji nishati ya umeme.


Mpaka mwaka ujao mpango huu utakuwa umetekelezwa katika shule 12 kwenye makambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya,Nyarugusu nchini Tanzania na Demokrasia ya Congo na utatoa elimu bora kwa watoto wapatao 15,000 wenye umri kati ya miaka 7 -20 .

Mpango huu tayari umeonyesha mafanikio makubwa ambapo mnamo mwaka 2014 taasisi ya Vodafone Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR limeweza kutoa elimu kwa watoto wapatao 18,000 kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya na walimu waliokuwa wanaendesha mafunzo chini ya mpango huu  wanakiri kwamba umeonyesha kuwa na  mafanikio na wanafunzi wameupenda na wameweza kupata elimu bora.


Katika kipindi cha miaka miwili ijayo mpango huu utatekelezwa katika makambi mbalimbali ya wakimbizi nchini Kenya,Tanzania na Demokrasia ya watu wa Congo lengo kubwa likiwa ni kuwafikia watoto 40,000 wanaoishi kwenye makambi ya wakimbizi.



Akiongea juu ya mradi huu Mkurugenzi wa taasisi ya Vodafone Foundation anasema: “Hadi mwaka 2013,UNHCR ilitoa takwimu  kuwa inakadiriwa kuwa kuna wakimbizi kwenye kambi mbalimbali duniani wapatao milioni 50 na kati yao nusu yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18 na hali hiyo inasababisha wapoteze ndoto ya kupata elimu.Mpango wa madarasa ya fasta wa Vodafone ni tumaini jipya na utawezesha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kama haya kupata elimu”.


Naye Afisa Mwandamizi wa UNHCR Olivier Delarue anasema:Kutokana na  majanga yanayojitokeza  na kusababisha kundi kubwa kuishi nje ya utaratibu wa maisha yao ya kawaida,UNHCR inakabiliwa na changamoto mbalimbali kuwapatia mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo elimu.Tunakaribisha ubunifu huu wa taasisi ya Vodafone katika kutoa elimu kwa wakimbizi na tuko tayari kufanya kazi na taasisi hii katika kukabiliana na changamoto nyingine tunazokabiliana nazo.”

No comments: