Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto)
akimsalimia mtumishi wa Wizara hiyo, Said Ngovi ambaye ni mvuta kamba wa timu
ya Utawala wakati Mkurugenzi huyo alipokuwa anazikagua timu mbalimbali za
wizara hiyo katika Tamasha la Michezo la kwanza lilishirikisha Wizara pamoja na
taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji,
Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika
katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Kapteni wa timu ya wanaume (Utawala) ya kuvuta kamba, Ally Lubuva.
Kapteni wa Timu ya Utawala ya kuvuta kamba
wanaume, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Chilipweli (kushoto)
akiimasisha timu yake kuivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo
zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na
wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya
mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha
Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza,
Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika
katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mary Nyegazeni akiishangilia timu yake ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume baada
ya kunyakua pointi mbili kwa kuivuta timu ya Uhamiaji katika mashindano maalumu
ya Tamasha la Michezo la wizara hiyo ambalo lilishirikisha Wizara pamoja na
taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji,
Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika
katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Amina Mavengero (katikati) akicheka kwa furaha baada ya
kushinda mchezo wa kufukuza kuku kwa kuwapiku wenzake wa Timu ya Utawala, Mary
Nyegazeni (kushoto) na Consalva Nagamchonga wa Timu ya Jeshi la Magereza.
Mchezo huo ulishirikisha watumishi wenye umri zaidi ya miaka 55 katika timu
zote zilizoshiriki. Wizara hiyo pamoja
na Taasisi zake za Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zilifanya mashindano ya michezo
mbalimbali yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga
jijini Dar es Salaam, ambapo Tamasha hilo lilifunguliwa na Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa.
Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanawake, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu
hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na
wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya
mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo
lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi,
Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizungumza na wanamichezo wa timu za
Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) walioshiriki katika michezo ya Kuvuta
kamba, mpira wa miguu, riadha, Netiboli na kufukuza kuku katika Tamasha kubwa
la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kuwakutanisha watumishi
wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo lilifanyika katika
Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya, na kulia ni Jesuad
Ikonko, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto), Kamishna
wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa (wapili kushoto) wakijumuika
kulisakata rumba na wanamichezo wa Wizara na Taasisi zake katika Tamasha la
Michezo la kwanza lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga
jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo lilijumuisha timu za Utawala, Jeshi la
Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida).
Katibu wa Michezo wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Jarahi Kilemile akimshukuru Mgeni rasmi ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Lilian Mapfa (hayupo pichani) kwa kulifungua na kufunga Tamasha kubwa la michezo
la wizara hiyo lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza,
Ukonga jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo lilijumuisha timu za Utawala,
Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida). Picha zote
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment