Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili Mahakama ya Wilaya Sikonge mkoani Tabora, katika Mahakama hiyo Mje. Jaji Mkuu alipata fursa ya kuongea na Watumishi ambapo aliwasisitiza kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi na taratibu za Kimahakama ili kutimiza wajibu wa utoaji haki sawa kwa wananchi. Kulia ni Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, kushoto ni Mhe. Sam Rumanyika, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akipanda mti wa kumbukumbu katika Mahakama ya Wilaya ya Sikonge iliyopo mkoani Tabora, Mhe. Jaji Mkuu alitembelea Mahakama hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama mkoani humo.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama wa Wilaya ya Sikonge iliyopo Mkoani Tabora alipotembelea Mahakama hiyo wikiendi.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga alipowasili mkoani humo kwa ziara ya Siku mbili.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania,akiongozana na Mtaalam kutoka TBA alipokuwa akikagua jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga lililopo katika hatua za mwisho za ujenzi, ukamilishwaji wa jengo la Mahakama Kuu Shinyanga utawezesha Mkoa huo ambao hutegemea Mahakama Kuu Tabora, kuwa na Mahakama yake na hatimaye kupunguza mlundikano wa kesi uliopo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania.)
No comments:
Post a Comment