Tuesday, March 17, 2015

jamii inapaswa kuwekeza katika sayansi na teknolojia - Balozi Sefue

Na May-Zuhura Simba

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii iweze kukua kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika sayansi na teknolojia.

Aliongea hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

“ubunifu katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika kupata uvumbuzi wa vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa jamii husika hivyo kuna umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi ili kupata matokeo mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue.

Aidha aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza katika sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa jamii zao.

Vilevile alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia katika kuleta mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu, afya,biashara,kilimo na miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya kijamii.

“Mfano mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania waliokuwa wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia sayansi na teknolojia ” alisema Balozi Sefue.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi, na serikali kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi zitakavyosaidia vijana kuvumbua teknolojia mbalimbali.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa warsha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu(kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John Mngodo,warsha hito iliandaliwa iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia John Mngodo akiwasalimia wajumbe wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kushoto ni Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede .
Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede, akiwasalimia wajumbe wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na wa mwisho kulia ni Naibu katibu Mkuu waWizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngodo .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, akisema hotuba ya kumakribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali ambao ni wajumbe wa mkutano wa ubunifu wa sera ya taifa ya Sayansi na teknolojia ilifanyika katika hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia.(Picha na Lorietha Laurence- Maelezo)

No comments: