Monday, February 2, 2015

WAZIRI WA UJENZI AFUNGUA BARABARA YA IGAWA-RUJEWA KM 9.8

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa barabara ya Igawa-Rujewa KM 9.8 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Mbarali.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara hiyo. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na viongozi wengine.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na wakazi wa Ubaruku wilayani Mbarali waliokuwa wanaomba wajengewe barabara ya Rujewa-Ubaruku kwa kiwango cha lami.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katikati akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kuhusu ujenzi wa barabara ya Rujewa-Ubaruku inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inatarajiwa kuwarahisishia wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wa mpunga na mahindi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku wilayani Mbarali kuhusu ujenzi wa barabara ya Igawa-Ubaruku km 18.
Wakazi wa Rujewa na Ubaruku wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi wakati akiwahutubia.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifurahia ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Rujewa mara baada ya kuwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwahutubia wakazi wa Ubaruku na Rujewa Wilayani Mbarali.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Igawa-Ubaruku inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wakazi wa Rujewa na Ubaruku mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

1 comment:

Anonymous said...

Ndugu waziri wa ujenzi, iangalieni barabara ya Iyunga to Iwambi upande wa Iyunga secondary. Nafikiri ile barabara ikiwekwa lami itakuwa msaada mkubwa wa kupunguza msangamano wa magari kutokea Iyunga kuelekea Mbalizi. Ile barabara ni muhimu sana pamoja na kwamba hakuna hata mmoja anayeifikiria. Sijui madiwani wa sehemu zile wanaonaje hilo.