Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Hawa Ghasia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa bodi
mpya ua wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa, akizungumza katika hafla hiyo. |
Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka akichangia jambo kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga akizungumza machache kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa
(kulia), akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia picha yenye nembo ya mfuko
huo kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa
LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya
mfuko huo Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa
(kulia), akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka picha
yenye nembo ya mfuko huo kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya
wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake
iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. Kushoto ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Hawa Ghasia.
Wajumbe wa bodi ya LAPF iliyomaliza muda wake.
Wajumbe wapya wa bodi ya LAPF
Mgeni
rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa),
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya zamani ya LAPF
iliyomaliza muda wake. Kushoto kwa waziri Ghasia ni Waziri wa Kazi na
Ajira, Gaudentia Kabaka ambaye wizara yake inasimamia mifuko hiyo ya
kijamii.
Mgeni
rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa),
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa bodi ya LAPF.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
…………………………………..
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Hawa Ghasia ameitaka bodi mpya ya Mfuko wa LAPF kufanyakazi
zao kwa maslahi ya mfuko huo badala ya kupendelea taasisi walizotoka.
Hayo
aliyasema wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya
mfuko wa Pensheni wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake
iliyofanyika makao makuu ya LAPF Dar es Salaam jana.
” Bodi hii mpya imeundwa katika mfumo wa utatu.
Kwanza
kuna wajumbe ambao wanatoka serikalini, pili wanaotoka chama cha
waajiri, na tatu wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi hivyo ninyi
wajumbe.
mna hadhi sawa katika utoaji michango itakayosaidia kuboresha shughuli za Mfuko” alisema Ghasia.
Ghasia
alisema wajumbe hao wote shughuli yao na lengo lao ni moja, nalo ni
kusimamia malengo na kazi za mfuko na kuhakikisha wanaasimamia maslahi
ya mfuko na siyo eneo ambako kila mmoja wao anatoka.
“Kwa
maneno mengine msifanye kazi kimajimbo”, kwani kufanya hivyo, kutaleta
migongano isiyo na tija na kuzorotesha ustawi wa mfuko, ambao kwa sasa
ndio mfuko wa hifadhi ya jamii unaokua kwa kasi zaidi nchini” alisema
Ghasia.
Alisema
anaamini wajumbe hao wote wameteuliwa kwa nia moja moja ya kuhakisha
mfuko huo unaongezeka hadi kufikia kilele cha mafanikio cha kuigwa hapa
nchini na pengine nje ya nchi na hiyo ndiyo imani kubwa ambayo Rais
Jakaya Kikwete anayo kwa LAPF.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Udhamini wa mfuko huo Profesa, Hasa Mlawa alisema michango
ya wanachama imekuwa ikiongezeka pia kwa kiwango cha kuridhisha ambapo
mwaka 2011 mfuko ulikusanya Sh. 80.5 bilioni na kiasi hicho kimeongezeka
hadi kufikia Sh. 157.6 bilioni mwezi Juni 2014 sawa na ongezeko la
asilimia 95.9 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Alisema
mambo yaliyofanya kiwango cha michango kuwa juu ni pamoja na ongezeko
la wanachama, mishahara, na uwasilishaji wa wakati unaofanywa na waajiri
na kuwa kutokana na michango hiyo fedha zilizowekezwa katika
vitegauchumi mbalimbali nazo ziliongezeka toka Sh. 387.6 bilioni mwezi
Juni 2011 hadi Sh. 748.67 bilioni mwezi Juni 2014 sawa na ongezeko la
asilimia 93.2.
Waziri
wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka ambaye mifuko hiyo ya jamii ipo chini
ya wizara yake alisema Serikali itaendelea kulipa madeni yanayodaiwa na
mifuko hiyo ili kuifanya iweze kuendelea.
No comments:
Post a Comment