Friday, February 20, 2015

VIONGOZI MBALI MBALI WAUWAGA MWILI WA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN BARAZA LA WAWAKILISHI,ZANZIBAR LEO

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowasa akiingia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kuuwaga mwili wa aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Marehemu Salmin Awadh Salmin aliefariki ghafla jana.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kuuwaga mwili wa Marehemu Salimn Awadh.
Mwili wa Marehemu Salmin Awadh ukiingizwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kuagwa rasmi.
Viongozi mbali mbali wakijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoa heshma za mwisho kwa marehemu Salmin Awadh Salmin katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akiongoza waumini katika Sala ya Marehemu Salmin Awadh Salmin katika Masjid Noor Muhammad (SAW) uliopo Mtaa wa Kwamchina mwanzo.
Viongozi mbali mbali akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Muhammed Shein wakimuonbea dua Marehemu Salmin Awadh baada ya sala iliyofanyika Masjid Noor Muhammad (SAW).
Viongozi walioshiriki sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiagana baada ya kumalizika sala hiyo.
Naibu Katibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mahmoud Muhammed wakibadilisha mawazo kuhusu msiba huo.
Mamia ya wananchi waliohudhuria sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiutoa msikitini mwili wa marehemu kuelekea kijijini kwao Makunduchi kwa mazishi.
Msafara uliobeba mwili wa Marehemu Salmin ukiondoka Masjid Noor Muhammad (SAW) kuelekea Makunduchi kwa ajili ya mazishi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments: