UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUHUSU MAOMBI YA TPDC YA TOZO ZA HUDUMA ZA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI
ASILIA
1.
Tarehe 1 Septemba 2014, Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata
na kusafirisha Gesi Asilia, na mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji
wa gesi asilia.
2.
Kati ya Septemba 2014 na Januari 2015,
EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha
gesi asilia, muundo wa mtaji (capital
structure) na faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa
mradi, pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.
3.
Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba
EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo:
(a) kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na
kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;
(b) tozo kwa huduma ya kuchakata na
kusafirisha gesi asilia iwe Dola za
Marekani 4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;
(c) faida kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane
(18%) na muundo wa mtaji wa asilimia
hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na
(d) mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa
ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa
kwa EWURA.
4.
Kwa mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha
Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014,
EWURA ilianza mchakato wa taftishi kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu
uhalali wa ombi lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja
mbalimbali ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la
Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican Energy
Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya Fedha, Wizara ya
Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za wadau na ufafanuzi
uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika kutoa uamuzi wa ombi hilo.
5.
Tarehe 8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano
na wadau wa karibu (Exit Conference) ambapo
EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata
maoni ya mwisho; na mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini,
Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC.
Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la EWURA. Kwa
ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika mikutano hiyo na hatimaye
kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC.
6.
Katika kikao chake cha tarehe 19
Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya
EWURA, ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha
miezi mitatu (Interim Tariff) ambacho
TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA
iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa ni kama ifuatavyo:
(a)
kanuni ya kukokotoa tozo za kuchakata
na kusafirisha gesi asilia iliyoombwa ilirekebishwa na kupitishwa ili itumike
kwa miaka 20 kuanzia mwezi Aprili 2015, na kurekebishwa kila baada ya miaka mitano;
|
|
(b)
gharama za Mradi wa Bomba la
kusafirisha gesi asili kutoka
Mtwara-Dar es Salaam zilizopitishwa ni sawa na Dola za Marekani 1,331.51 milioni, ambapo gharama hizi zitabaki
hivyo hadi mwezi Juni 2015 ambapo gharama halisi za mradi zitakapojulikana na
kufungwa;
(c)
gharama za uendeshaji zitakuwa sawa
na Dola za Marekani 241.58 milioni
kwa mwaka;
|
|
(f)
tozo ya kuchakata na kusafirisha gesi
asilia italipwa kwa Shilingi za Tanzania, kwa kiasi sawa na jumla ya Dola za Marekani 2.14 kwa uniti,
ambapo tozo ya kuchakata gesi asilia itakuwa Dola za Marekani 0.95 kwa uniti.
Kati ya hizo, na tozo la kusafirisha gesi asilia itakuwa Dola za Marekani
1.19 kwa uniti. Tozo hizi zitatumika hadi hapo EWURA itakapotoa agizo lingine
baada ya kutathmini gharama halisi za mradi zitakapojulikana na ujenzi
kukamilika;
(g)
endapo EWURA haitatoa agizo
jingine, tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia kama zinavyoonekana
kwenye aya ya 6(f) hapo juu zitaendelea kwa miaka mitatu (Aprili 2015 hadi
Juni 2018);
(h)
faida kwenye mtaji ya asilimia 4.58 na uwiano wa mtaji wa asilimia 75
fedha za mkopo na asilimia 25 fedha za TPDC (75:25); na
(i)
mwezi Septemba kila mwaka wa tatu,
utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata
yatawasilishwa kwa EWURA.
|
|
7.
Pamoja na maamuzi hayo hapo juu, TPDC
wanaagizwa kutekeleza masharti yafuatayo:-
|
|
(a)
kuzingatia kanuni za ushindani kama
zilivyoainishwa katika Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 (Public Procurement Act, 2011) na
kuiarifu EWURA kila TPDC inapofanya manunuzi ya thamani yanayozidi dola za
Marekani 5 milioni.
(b)
endapo kuna ulazima wa kutumia
utaratibu wingine kwa mujibu wa Sheria,
ndani ya siku thelathini (30) baada ya kuingia mikataba ya manunuzi TPDC italazimika
kutoa taarifa na kuwasilisha nakala za mikataba EWURA;
|
|
(c)
ndani ya kipindi cha miezi kumi
na miwili (12) baada ya Agizo la EWURA, kuwasilisha EWURA, mpango wa
uendelezaji wa miundombinu ya gesi asilia (the Natural Gas Infrastructure Development Plan);
(d)
ndani ya kipindi cha miezi kumi
na miwili (12) baada ya Agizo la EWURA,
kuwasilisha EWURA, mpango wa utumiaji wa miundombinu ya gesi asilia iliyojengwa
(the Natural Gas Infrastructure
Utilisation Plan);
|
|
(e)
ndani ya kipindi cha miezi kumi
na miwili (12) tokea kuanza kwa Agizo la EWURA, kuandaa Mkataba wa Huduma kwa
Wateja, ili kupima ufanisi katika kutoa huduma za usambazaji wa gesi asilia
na kushughulikia malalamiko ya wateja.
(f)
kuhakikisha kwamba mfuko wa
dhamana kwa ajili ya manunuzi ya gesi kutoka kwa wawekezaji wenye visima vya
gesi asilia unakuwa wa kiasi cha fedha kisichopungua Shilingi 153 bilioni kila
wakati kwa kipindi chote cha mradi; Aidha;
(g)
Kabla ya kuanza kutumika kwa
Mkataba wa Huduma kwa Wateja, kuwasilisha mkataba huo EWURA kwa ajili ya
kuupitisha; na
Agizo hili litaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 APRILI
2015
IMETOLEWA NAFELIX NGAMLAGOSI
MKURUGENZI
MKUU
20
FEBRUARI 2015
|
|
|
No comments:
Post a Comment