Saturday, February 21, 2015

DKT.SHEIN, DKT. BILAL WAONGOZA MAZISHI YA MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI SALMIN AWADHI SALMIN, MAKUNDUCHI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza wananchi kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Unguja, aliyefariki ghafla jana wakati akiwa katika kikao cha Chama Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana Feb 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Shein, wakiwaongoza baadhi ya viongozi wa Serikali na wananchi wakati wa kuswalia mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Unguja, aliyefariki ghafla jana wakati akiwa katika kikao cha Chama Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana Feb 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, wakati walipokutana katika swala maalum ya kumswalia aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyefariki jana ghafla akiwa katika Kikao cha Chama Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, wakati walipokutana katika swala maalum ya kumswalia aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyefariki jana ghafla akiwa katika Kikao cha Chama Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati walipokutana katika shughuli za maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyefariki jana ghafla akiwa katika Kikao cha Chama Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Magige Nyerere, wakati walipokutana katika shughuli za maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, huko Makunduchi mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa juu wa Serikali, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, huko Makunduchi mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa leo Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
Makamu wa pili Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015. Picha na OMR

No comments: