Mkuu wa wilaya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Kiislamu, Twayyibat, iliyopo Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.
Kuwapo kwa
shule hizo kutazidi kuongeza idadi kubwa ya watoto wanaopata elimu ya msingi,
sekondari na vyuo Vikuu kwa ajili ya kujikomboa katika maisha yao.
Ukiacha
mikoani ambako hakuna shule nyingi hususan maeneo ya vijijini, jijini Dar es
Salaam kumefanikiwa kuwa na shule nyingi mno, zikiwamo za serikali na
mashirika.
Zipo shule
za kidini ambazo wakati wote zimekuwa zikifundisha watoto elimu ya Dunia na ile
ya kufahamu Mungu ni nani, nazumgumzia pale watoto wanapofundishwa kisawa sawa
na kukolea kiimani kama njia ya kumjua Mungu na kutenda matendo ya kiungwana.
Mwishoni mwa
wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, alitembelea katika shule
ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.
DC Sofia
alitumia muda huo kuikagua shule hiyo pamoja na kuzungumza na wadau wa elimu,
walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya kuona inakuwa kati ya shule bora
wilayani Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla.
Miongoni mwa
mambo yaliyomkosha DC Sofia ni pale alipoambiwa kuwa ada ya shule hiyo kwa
mwaka mmoja ni Sh 200,000 tu, jambo ambalo ni agharabu kuliona wala kulikisia
katika shule mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
shuleni hapo, Mkuu huyo wa wilaya ya Temeke, Sofia, anasema kwamba ameshangazwa
na kuwapo kwa ada nafuu katika shule ya Twayyibat.
“Hili bado
linanifanya nijiulize urahisi wa ada hizi wakati najua fika siku hizi elimu ni
ghari na kuna mambo mengi yanayohitajika ili shule ziweze kujiendesha, ikiwamo
mishahara ya walimu.
“Katika hili
linanifanya nione serikali hususan Halmashauri ya wilaya ya Temeke inakaa na
viongozi wa shule hii kutatua changamoto zinazowezekana kwakuwa kwa ada hizi
shule haiwezi kujiendeshaa vizuri na kusonga mbele,” alisema.
DC huyo
anasema urahisi wa ada hizo katika shule ya Twayyibat sit u utawafanya wazazi
na walezi wamudu kusomesha watoto wao, bali pia kukuza kiwango cha elimu cha
Temeke na Tanzania kwa ujumla.
Anasema
amefurahishwa na mazingira ya shule hiyo, ingawa hajaona maabara, jambo
alilojibiwa na uongozi wa shule kuwa tayari wameshatenga eneo la kujenga
maabara kwa ajili ya shule hiyo ya sekondari ya Kiislamu.
“Maabara ni
muhimu mno, fanyeni kila liwezekanalo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inakuwapo,
maana kama tungewasiliana kwa karibu na Halmashauri yetu ni wazi tungeangalia
namna ya kusaidia katika hilo ukizingatia kuwa shule inatoa huduma na ada zake
ni nafuu.
“Tukitoka
hapa tutafute namna bora ya kuhakikisha kuwa shule hii inakuwa bora, kwakuwa
nimeshaona misingi na dhamira ya kweli kutoka kwa walimu, wadau, viongozi na
wanafunzi kwa ujumla ili kuwapa mwanga zaidi, alisema.
DC Sofia
aliwasili shuleni hapo saa 7 mchana, huku akipokewa kwa shangwe na wanafunzi wa
shule hiyo, wadau wa elimu na wahisani wa shule hiyo, bila kusahau walimu
waliokuwa na shauku ya kumpokea mgeni huyo tangu asubuhi.
Baada ya
kuingia na kusaini kitabu cha wageni, alianza kutembezwa katika eneo lote la
shule hiyo na kujionea hali ya kielimu inavyoendelea na namna wanavyofanya kazi
zao.
Akizungumzia
hali yaa utendaji kazi na uwajibikaji kwa walimu hao, DC Sofia aliwataka walimu
kuongeza bidii ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wao wanafanya vizuri katika
mitihani ya Taifa ya kidato cha nne.
Anasema
shule ina matokeo ya kuridhisha kutokana na wanafunzi wao kujisomea vizuri,
wakiamini kuwa ni elimu pekee ndiyo inayoweza kuwakomboa katika maisha yao.“Nashauri
wanafunzi waelimishwe zaidi umuhimu wa kujisomea ili waachane na mambo ya
Kidunia wakiwa bado wadogo kwakuwa wataharibu maisha yao.
“Mambo ya
anasa na starehe zisizokuwa na tija zimepitwa na wakati kwakuwa wanaweza
kuharibu kabisa mfumo wao wa maisha na kujiweka katika kundi la majuto,”
alisema.Aidha DC
huyo alitumia muda huo kuwapongeza wahisani na wadau mbalimbali wanaoiwezesha
hiyo yenye maskani yake wilayani Temeke, karibu na Msikiti wa Tungi.
Pia
aliwakabidhi wahisani hao vyeti vya kutambua mchango wao kutokana na mara kwa
mara kujitolea misaada mbalimbali inayochangia maendeleo ya kielimu kwa shule
hiyo.
Baadhi ya
wahisani waliokabidhiwa vyeti hivyo ni pamoja na Adam Malima, Skywards
Construction, Shaimar Kweigir, Zainabu Vullu, Yakubu Chamber&Associate,
Alosco, Home Shooping Centre, ambapo baadhi yao waliwakilishwa kutokana na kuwa
na majukumu mengine ya kiserikali.
Naye Mkuu wa
Shule hiyo, Juma Omari, anasema shule yao imekuwa na mafanikio makubwa kutokana
na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi
kuwapa mwanga wa kielimu watoto wanaosoma Twayyibat.
“Tangu shule
hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na matokeo
yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze bidii katika kufundisha wanafunzi wetu
tukiamini ndio mpango sahihi.
“Sisi kama
walimu tumekuwa tukiongeza bidii katika ufundishaji kwa ajili ya kuhakikisha
kuwa shule yetu inakuwa bora kati ya nyingine, huku tukiamini kuwa kwa pamoja
tutakuwa tunazifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazotukabili,” alisema.
Mkuu huyo wa
shule aliwataka wazazi na walezi kuacha sababu, maanaa shule yao inafikika
kiurahisi na imeamua kutoza ada nafuu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto
wote wanapata haki ya kupata elimu.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.
1 comment:
Ni jambo la kupigiwa mfano. Hongera sana wafadhili na wadau wengine wa shule
Post a Comment