Thursday, February 5, 2015

KILIMANJARO WALIVYO SHEREHEKEA SIKU YA SHERIA NCHINI 2015.

Brass Band ya Chuo cha Polisi Moshi ikiongoza maandamano siku ya Sheria nchini kwa mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya Wanasheria ,Mahakimu na watumishi wa Mahakama wakiwa katika maandamano hayo yaliyopita katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
Askari wa Kikosi cha kutuliza wakiwa tayari kwa ajili ya gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya siku ya Sheria nchini iliyadhmishwa Mahakama kuu kanda ya Moshi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akiongoza wageni wengine kuelekea katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi kwa ajili ya kukagua gwaride la heshima. 
Askari wakiwa timamu kwa ajili ya gwaride la heshima mbele ya jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari.(hayuko pichani)
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akipokea salamu za heshima toka kwa askari Polisi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya siku ya sheria.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Sheria ambayo kwa mkoa wa Kilimanjaro yameadhimishwa katika mahakama kuu kanda ya Moshi.
Baadhi ya Mawakili wa serikali na wale wa kujitegemea wakifuatilia tukio hilo.
Baadhi ya Mahakimu wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi.
Jaji Mfawidhi Sumari akiwaongoza wageni wengine kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya wageni .
Baadhi ya wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo watumishi wa mahakama wakifuatilia tukio hilo.
Msajili wa Mahakama mkuu kanda ya Moshi,Hussein Mushi akisherehesha sherehe ya maadhimisho ya siku ya sheria iliyofanyika kimkoa katika mahakama kuu kanda ya Moshi.
Baadhi ya wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.
Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi ,Munga Sabuni na mwenzake Julieth Mawole wakiwa katika viunga vya mahakama Kuu kanda ya Moshi.
Baadhi ya Mahakimu na watumishi wa mahakama wakiwa katika sherehe hizo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiteta jambo na jaji mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya moshi,Alishaeli Sumari wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo.
Baadhi ya waviongozi waliokuwa meza kuu .
Mawakili wakifuatilia kwa karibu tukio hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanzania Bara tawi la Moshi ,David Shilatu akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika kwa mkoa wa Kilimanjaro , mahakama kuu kanda ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiteta jambo na Jaji Benedict Mwngwa wakati wa sherehe hizo.
Mwanasheria Mfawidhi wa serikali ,Neema Mwanda akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria nchini ambayo kimkoa yamefanyika katika viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa salamu zake katika maadhimisho hayo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini.
Kikundi cha burudani ya ngoma cha Msanja hakikuwa nyuma katika utoaji wa burudani.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: