Thursday, February 5, 2015

KAIRUKI HOSPITALI YAINGIZA MTAMBO MAALUMU WA UPASUAJI

HOSPITALI ya Kumbukumbu ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, imeingiza mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya Marekani utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa  kawaida na ule matobo.
 Mtambo huu unafahamika  kama Ultrasonic and Advanced Bipolar HARMONIC Generator unatumia nishati ya sauti au mwangwi (ultrasound) kuweza kukata mwili wa binadamu bila kupoteza hata chembe ya damu kwa mgonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Upasuaji katika hospitali hiyo, Dk. Muganyizi Kairuki alisema kuwa mtambo huo unaweza kupunguza athari zinazoweza kutokea kwa viungo vya jirani wakati wa upasuaji kama ilivyo kwa mitambo ya  zamani inayotumika sasa katika hospitali nyingine. 
Dk. Muganyizi aliongeza kuwa faida za mtambo huo ni 
kurahisisha na kuharakisha upasuaji hivyo kupunguza muda wa upasuaji kwa jumla na kuondoa kabisa matumizi ya nyuzi  za kushonea viungo vya ndani wakati wa upasuaji. 
 "Mtambo huo unapunguza matumizi na mahitaji ya damu ambayo ni adimu kupatikana kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji hospitalini". alisema Dk. Muganyizi.
Mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya  Marekani  utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa    kawaida na ule wa matobo.

No comments: