Na
Bashir Yakub.
Yapo
mambo ambayo huwaumiza watu vIchwa
yumkini yakiwa ni mambo madogo na ya kawaida. Tatizo mara nyingi huwa ni taarifa. Taarifa zikimfikia
mtu ndipo huhisi jambo ambalo
alikuwa halijui kuwa ni jepesi. Lakini
kabla ya taarifa mtu huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu.
Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la anasa
au ufahari tena isipokuwa ni jambo
ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida ya
kila siku ya walio wengi. Hii ni kutokana na kukua kwa biashara za kimataifa, mawasiliano,
utalii,usafirishaji na kila kitu ambacho
husababisha watu kutoka nchi moja hadi
nyingine. Kwasasa kuwa na pasipoti hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo
muhimu sana. Yumkini usisubiri ikutokee
safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana
na pasipoti. Pasipoti inayo
manufaa mengi lakini moja ni kuwa
pasipoti ni mali kama mali nyingine.
Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama mali
nyingine inavyoweza kumdhamini mtu.Pasipoti ni amana tena amana ya kuaminika. Ni kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze pasipoti na namna ya kupata pasipoti.
1.
PASIPOTI HUOMBWA
NA MWOMBAJI LAKINI HUBAKI
MALI YA SERIKALI.
Hakuna
mtu mwenye umiliki wa kudumu wa pasipoti.
Kwa mujibu wa sheria licha ya kuwa pasipoti hutolewa kwa jina na maelezo ya
mwombaji,hati hiyo hubaki kuwa ni mali ya serikali. Hii ndio sababu serikali
huweza kumnyanganya mtu pasipoti panapo jambo fulani. Ni kwakuwa
pasipoti ni mali yake. Wewe mwombaji
uliyepewa pasipoti unayo haki ya
matumizi na uhifadhi wake lakini mmiliki mkuu ni serikali.
2.
ILI
KUPATA PASIPOTI UNAHITAJI
KUWA NA VITU HIVI.
( a ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa
kuandikishwa cha mwombaji.Cheti cha kuzaliwa
ni hivi vyeti vya kawaida ambavyo hutolewa mahospitalini
au mamlaka nyingine baada ya
kuzaliwa kwa mtu. Katika kipindi hiki wapo wengine wamekwisapata vyeti vya uraia. Cheti cha uraia chaweza kutumika kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa.
Pia tumesema hati ya kiapo. Hii hutolewa kwenye ofisi za wanasheria. Mwombaji
huwa anaapa pamoja na mambo mengine
kuthibitisha kuwa taarifa anazozitoa
ni za kweli kwa dhati yake. Pia tukasema vyeti vya uraia wa kuandikishwa.
Hivi wanavyo raia wa Tanzania ambao si wa kuzaliwa. Katika kuomba kupata
pasipoti nao hutakiwa kuwa navyo.
( b ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa
kuandikishwa cha
mzazi au wazazi wa mwombaji. Hapo juu tumeona vitu kama hivihivi lakini ilikuwa ni kwa mwombaji wa pasipoti mwenyewe.
Hivi hapa sasa ni kwa ajili ya mzazi wa mwombaji. Vile vitu
vyote alivyowasilisha mwombaji pale juu ndio
vilevile anavyopaswa kuwasilisha
mzazi wa mwombaji. Si kwamba mzazi mwenyewe ndio anapeleka vitu hivyo hapana,
wewe mwombaji ndio unabeba vitu hivi kwa niaba ya mzazi. Hapa mzazi ni yeyote
anaweza kuwa baba au mama.Lengo lake ni
kutaka kujua historia fupi ya nasaba ya mzazi wa mwombaji.
( c ) Inahitajika picha ya hivi karibuni ya pasipoti size. Sharti
kubwa waliloweka hapa ni kuwa picha hiyo
isiwe katika fremu. Fremu hapa si tu ile fremu ya kawaida tuliyoizoea bali pia
hata pasipoti kuwa na maringo au mapambo ya kuzungushia pembeni nayo ni fremu
kwa maana hii. Pasipoti iwe mnyooko(plain) isiwe na mbwembwe zozote.
( d ) Iwapo mwombaji ana umri wa chini ya miaka kumi na nane
(18), wazazi
walezi wawasilishe ridhaa ya maandishi. Nyaraka
hii ya ridhaa ya maandishi huandaliwa
na mwanasheria.Hii ni kusema kuwa utaratibu wa mtu mzima aliyevuka miaka
kumi na nane ni tofauti na mtu aliye
chini ya miaka hiyo katika kupata
pasipoti. Baada ya kukamilisha vitu hivi kama
nilivyoeleza basi hatua
inayofuata ni kufuata utaratibu huu chini.
3.
FOMU ZA MAOMBI HUPATIKANA WAPI.
Ofisi za uhamiaji ndipo zilipo fomu za maombi ya pasipoti. Hii ni popote Dar es salaam au mikoani. Suala la msingi
ni kuwa ofisi hiyo iwe ya uhamiaji
utapata fomu hizo. Utachukua fomu hiyo utaijaza na baada ya kuijaza itawasilishwa kwa
mkurugenzi wa uhamiaji. Aidha suala jingine la msingi ni kuwa fomu hii
itawasilishwa sambamba na nyaraka zote zinazotakiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.
4.
BEI
YA PASIPOTI NI
KIASI GANI.
Ada
rasmi ya kupata pasipoti ni fedha za Kitanzania kiasi cha shilingi 50,000/=(
Elfu hamsini tu). Aidha kwakuwa wanasheria ndio hushughulika na kutafuta
pasipoti basi bei yao haiingizwi katika ada rasmi ya serikali kama
nilivyoieleza hapo juu.
5.
UNAWEZA KUOMBWA VIAMBATANISHO VYA ZIADA.
Jambo jingine ni kuwa safari zimeainishwa kwa namna
mbalimbali.Ukisoma nyuma ya fomu ya maombi utaliona hili. Kutokana na hilo wakati
mwingine waweza kuombwa viambatanisho vya ziada. Hii ni kutokana na utofauti wa
safari. Hii ni kusema kuwa yawezekana mwombaji akaombwa viambatanisho viitwavyo
viambatanisho “maalum”. Hivyo basi mtu asishangae kukutana na kitu cha namna
hiyo.
MWANDISHI
WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
No comments:
Post a Comment