Friday, February 6, 2015

Airtel yashirikiana na Kitengo cha damu salama cha taifa kuokoa maisha

Mtaalam wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Daudi Mkawa akimtoa damu Mfanyakazi wa Airtel Tanzania, Amitin Mbamba wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Adam Suleiman na Frank Munale wakitolewa damu kwa ajili ya kuchangia katika Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Mtaalam wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Judith Goshashy akimpima shinikizo la damu Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Mnasihi wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Julius Nkomwa akimtoa damu Mkurugenzi wa Fedha wa Airtel Tanzania, Ketan Mehta wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.

Airtel Tanzania imeshirikiana na Kitengo cha damu salama cha taifa (National Blood Transfusion Services) katika zoezi la kuchagia damu ili kupunguza upungufu mkubwa nchini ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwaajilii ya dharura za kitabibu kila mwaka.

Zoezi hilo la kuchangia damu limewashirikisha wafanyakazi wa Airtel kutoka katika vitengo mbalimbali kujitolea na kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia jamii.

Akiongea kwa niaba ya Airtel , Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema “ Airtel tunaamini katika kugusa maisha ya watanzania kwa njia mbali mbali huku tukishirikiana na wafanyakazi na wadau mbali mbali katika kufanikisha hilo. Tumekuwa tukishirikiana na Kitengo cha kuchagia damu kila mwaka kwa kuhusisha wafanyakazi na wadau mbali mbali kuchangia ili kuongeza damu katika benki ya damu ya taifa kwa ajili ya mahitaji ya dharura. Mwaka huu tunaendeleza utamaduni huu ili kuwawezesha matibabu hususani kwa wanawake na watoto wanaohitaji msaada wa damu kupata huduma hii kwa urahisi.

Tunawashukuru wafanyakazi na wadau wetu mbalimbali kwa kujitolea na kushiriki katika kuchangia kila mwaka na pia tunaahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii na wafanyakazi wetu juu ya umuhumi wa kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo tunaweza kuokoa maisha ya wengi wanaohitaji huduma hii kuipata kwa haraka na urahisi.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka kitengo cha damu salam Judith Charles alisema” Tunawashukuru wafanyakazi wa Airtel kwa kuonyesha mfano kwa kujitokeza kuchangia damu leo, Natoa wito kwa watanzania kujenga tabia ya kujitolea kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo kutatuwezesha kuwa na units za kutosha kuhudumia wale wanaohitaji wakati wa dharura. Maisha hayana uhakika inawezekana siku moja wewe ukawa ni mmoja kati ya wale wanaohitaji, hivyo tunahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia damu.

Mpaka sasa kitengo chetu kina tatizo la uhaba mkubwa wa damu hivyo natoa wito kwa watanzania mmoja mmoja au kwa makundi kujitokeza kuchangia ili tuwe na kiwango cha damu kinachokidhi mahitaji yanayokua kwa kasi kila siku.

No comments: