Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
wa pili kushoto akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng.
Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu ya ujasiriamali kwa
vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni
Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina
Sanga.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bi. Amina Sanga kulia akizungumza na vijana wa Wilaya ya Rungwe wakati wa semina ya
Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya
Rungwe. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi
Ester Riwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa
semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika
Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Kijana Daudi Essau Seme kutoka katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited
akichangia wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo
ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe katika kikundi wakijadiliana namna ya kuandika
andiko la mradi baada ya kuelimishwa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi
na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Kijana Daudi Essau Seme kutoka katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited
kushoto akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
walipotembelea mradi wa kikundi hicho wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya
ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza
kwa makini kijana Boniel Soka (kushoto) kutoka kikundi cha Muungano Makandana
kinachojishughulisha na upandaji miti ya aina mbalimbali wakati wa ziara ya kukagua miradi ya
vijana wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo. Rungwe, Mbeya
No comments:
Post a Comment