Saturday, January 24, 2015

WENGI JIJINI NEW YORK WAVUTIWA NA APP INAYOTANGAZA VIVUTIO VYA KITALII NCHINI TANZANIA

 App inayoonyesha vivutio mbalimbali vya kitalii  nchini Tanzania,  App hiyo ambayo imeandaliwa na Bi. Benita Cassar Torreggiani kwa  kusaidiwa na wataalam kutoka Apple  inaweza kupatikana kupitia  mitandao ya Ipad, Iphone na  Smart Phone. 
 Mfanyakazi wa Apple Store Grand Centra jijini New  York ambako onyesho hilo lilifanyika akimtambulisha Bi. Benita.
 Balozi Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa,  akizungumza  na Bi . Benita ambapo alimshukuru kwa uamuzi wake huo wa kutangaza utalii wa  Tanzania kupitia App hiyo.
 Sehemu ya wageni waaliwa waliofika kushuhudia onyesho la App hiyo  na ambao walielezea kuvutiwa sana na kila kilichopo katika App hiyo
 Balozi Manongi akuzungumza na wageni waliofika kwenye onyesho ambapo pia alijibu  baadhi ya maswali yao
 Hapa pia Balozi Manongi akiendelea na diplomasia ya  Utalii akiwatia shime wageni waliohudhuri onyesho hilo kwamba wasiishie kuangali App bali wafike  Tanzania washuhudie wenyewe.
 Wawakilishi Kutoka TANAPA   Dk. Ezekiel Dembe na Bw. Ibrahim Mussa ambao ni sehemu ya   ujumbe wa  Tanzania kwenye Onyesho jingine la masuala ya Utalii  maarufu kama  New  York Times Travel Show nao walijumuika na wageni wengine kuangalia onyesho la App destination Tanzania.
 Wageni wengine waalikwa
 . Balozi Manongi  akibadilishana  mawazo na wamiliki wa Kampuni ya Coastal Air Travel ambao wapo   hapa New York kushiriki onyesho la  New York Times Travel  Show
 Sehemu ya wagine wakifuatilia maelezo ya  App  hiyo kupitia screen zilizokuwa zilizowekwa  ukutani katika eneo palipofanyika onyesho hilo
Wageni waalikwa

No comments: