Vyombo
vya habari nchini vimehimizwa kuwasilisha masuala yanayowahusu watoto
yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Akizungumza na
wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha katika warsha juu ya
HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoendeshwa na shirika liliso la kiserikali la The Foundation For
Tomorrow (TFFT).
Mkurugenzi
Mkuu wa Tanzania wa shirika hilo, Bwa. Kennedy Oulu alisema tatizo la
watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu nchini Tanzania ni
gumu, hivyo vyombo vya habari havina budi kuifahamisha jamii kuhusu
hili suala na matatizo yanayowakabili watoto yatima na waishio katika
mazingira magumu ili jamii na wadau mbalimbali waweze kushiriki vema
katika kukabiliana na tatizo hili.
“Kwa
sasa, inakadiriwa kuwa kuna watoto yatima na wale waishio katika
mazingira magumu wapatao 1,800,000 hapa Tanzania pekee, huku 1,300,000
kati yao wakiwa wametokana na athari za ugonjwa wa UKIMWI. Mgawanyo wa
kifamilia na muundo wa kimsaada kijamii ni moja ya vinavyochangia tatizo
hili.
Vinapoongezwa katika umaskini unaojidhihirisha katika: ukosefu wa
upatikanaji wa huduma za elimu ikiwemo elimu ya awali, ukosefu wa
upatikanaji wa huduma za afya na uzalishaji kama afya ya uzazi, ukosefu
wa stadi za maisha zinazoakisiwa katika mitaala ya shule zenye uwezo
unaotakiwa na ubunifu ili kujenga uwezo wa watoto, si kwa yatima na
waishio katika magumu pekee”. Alisema Kennedy na kuongeza.
“Ni
muhimu kutambua kuwa kumekuwa na hatua na mafanikio yaliyofikiwa na
wadau mbalimbali ikiwemo serikali katika kuwezesha upatikanaji,
kuzijengea uwezo familia za watoto hawa na kubadili mitazamo ya jamii
dhidi ya watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu, hii
inajenga msingi wa mwitikio endelevu.
Kwa upande wake, shirika la The Foundation For Tomorrow limekuwa likilishughurikia tatizo hili kwa njia mbalimbali. Shirika hili hutumia njia anuai ambazo hupunguza uhitaji wa watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu kwa kuzijengea uwezo wa kiuchumi kaya zao hususani zile kaya maskini kupindukia, kutoa msaada wa kugharamia masomo ili kuwahakikishia upatikanaji wa elimu, kutoa bima za afya kwa wanafunzi yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu, kuwajengea uwezo walimu na kuwezesha stadi za maisha kwa njia ya kuboresha mtaala.
Bwa. Oulu amesema juhudi hizi pamoja na sauti za watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu zinapaswa kufahamika. “Changamoto za hawa watoto na mitazamo yao hutusaidia kutambua njia iliyo bora ya kulinda maisha yao. Hizo pia hutuwezesha kutambua kuwa kwa kiasi kikubwa sote tunalo jukumu la kubadili vile tunavyowachukia hawa watoto kutoka katika kudharauliwa na badala yake kuwa katika ufahamu kuwa sababu ya hali hizo na magumu yaliyopo ndiyo matatizo tunayoyashughurikia Tanzania yote: elimu, afya, umaskini, kaya na kufikia fursa zilizopo.”
Inapaswa
kuoneshwa ya kwamba hali hii lazima ionwe kuwa si ya kudumu wakati
hatua zinazochukuliwa, kujenga kipato baina ya kaya maskini, kuwezesha
upatikanaji wa mahitaji na kulinda haki na ulinzi kwa watoto, hususani
kwa kuwahakikishia elimu bora na ushiriki wao usio na kikomo ni muhimu
katika kutokomeza tatizo hili.
Bwa.
Oulu aliongeza kuwa “Uandishi wa habari wa kiuchunguzi na uwasilishaji
mambo wenye malengo, suluhisho, utendaji bora na juhudi zilizoshindwa
ndivyo vitaiwezesha jamii kujua ni njia gani bora ya kusaidia, kuitikia
na kudumisha juhudi na fursa za kuwaondoa watoto yatima na wale
wasiojiweza kutoka katika janga hilo. Inapaswa ioneshwe kuwa watoto
yatima na wale waishio katika mazingira magumu pamoja na wanaowahifadhi
na kaya zao wanayo hatua kubwa ya kuchukua.”
Sambamba na hilo, msimamizi wa warsha hiyo Bwa. Augustine Zacharia alivishauri pia vyombo vya habari kuzingatia ni jinsi gani habari zinazotolewa katika vyombo vyao huwaathiri watoto hawa kwa upande chanya na hasi. Masuala yahusuyo watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu yanapaswa kuwasilishwa katika namna ambayo huwajenga na kuwa katika mtazamo wa kutafuta suluhisho la tatizo. Licha ya kuwa kuna uhuru wa kutoa na kupokea habari, lakini namna ambavyo habari hizi huwasilishwa, zinapaswa kwanza kuzingatia kuwa haki za watoto hazivunjwi.
Meneja
wa ushirikiano wa The Foundation For Tomorrow Bw.Anton Asukile akiwa
anatoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari katika semina ya siku moja juu
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha
iliyofanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden jijini Arusha
Mwezeshaji
wa Semina juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA
MAZINGIRA MAGUMU Bw.Zachariah A.Babu akiwa anatoa maelekezo kwa waandishi
wa habari juu ya Haki ya watoto
Meneja
wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow
Bi.Melissa Queyquep akiongea katika warsha juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA
NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo
Mwenyekiti wa Arusha press club, Claud Gwandu
Mwandishi mwandamizi wa kituo cha Redio 5 David Rwenyagira akiwa anafwatilia mafunzo
Waandishi
wakiwa wanafatilia sema juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI
KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la
The Foundation For Tomorrow kulia ni Daniel Lucas mhariri wa Safina
Redio na Merry Mwita kutoka gazeti la Mtanzania
Kulia ni Queen Lema wa gazeti la Majira,Rose Jackson wa gazeti la jambo leo wakiwa katika semina hiyo
Waandishi kutoka Habari Maalum Media Arusha,kulia ni Daniel Magulu na Edith Laizer
Kushoto ni Jamillah Omar wa chanel Ten katikati Happy Lazaro wa mwananchi na Cynthia Mwilolezi wa gazeti la Nipashe
Kushoto Lilian Joel wa gazeti la Uhuru na Elia Mbonea wa gazeti la Mtanzania
Mwezeshaji
wa Semina juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA
MAZINGIRA MAGUMU Bw.Zachariah A.Babu akiwa anasisitiza jambo
Waandishi
mwandamizi Jamillah Omar wa chanel Ten akiwa anapokea cheti kutoka kwa
Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow
Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA
NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo
jijini Arusha
Mwandishi mwandamizi wa kituo cha Redio 5 David Rwenyagira akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwandishi kutoka Habari Maalum Bi.Edith Laizer akiwa anachangia katika semina hiyo
Mwandishi mwandamizi Queen Lema wa gazeti la Majira akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa libeneke la kaskazini Woinde Shiza akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mmiliki wa mtandao wa kijamii http://jamiiblog.co.tz/ Pamela Mollel akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwandishi wa Star TV Magessa Magessa akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwandishi wa mambo jambo redio Rotilinde Achimpota akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwandishi Peter Saramba wa Mwananchi akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwandishi kutoka gazeti la habari Leo Veronica Mheta akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Cynthia Mwilolezi wa gazeti la Nipashe akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Elia Mbonea kutoka Mtanznia akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Rose Jackson wa Jambo Leo akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Daniel Lucas mhariri wa Safina Redio akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwakilishi kutoka Habari Maalum Daniel Magulu akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwakilishi kutoka Habari Maalum Edith Laizer akiwa
anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The
Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina
ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
Mwenyekiti
wa Arusha press club, Claud Gwandu akitoa neno la shukrani kwa shirika
hilo kuandaa semina kama hiyo kwa waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment