Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza akiwakaribisha wajumbe
wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji waliotembelea mkoa
huo kukagua baadhi ya miradi ya Maji iliyopo mkoani humo.
Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo
na Maji, Amina Makilagi akieleza lengo la ziara ya kamati ya Bunge
ya Kilimo, Mifugo na Maji mkoani Mtwara kwa Mkuu wa mkoa huo
Mwantumu Mahiza (kushoto).Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Asaa
Hamadi.
Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo,
Mifugo na Maji, Amina Makilagi, akieleza jambo wakati alipowasili
kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Lindi tayari kukagua miradi
ya maji.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassor Himid na kulia ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Mathei Makwinya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Mathei Makwinya, akieleza
jambo wakati ziara ilipowasili kwenye kijiji cha Mnara kukagua mradi
wa Rondo-Mnara.Kulia kwake ni Kiongozi wa wajumbe wa kamati
ya Bunge, Amina Makilagi, Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassor Himid na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lindi Olliver Vavunge.
Baadi ya viongozi wa kijiji na kamati ya maji ya kijiji cha Mnara na
Chiponda wakimsikiliza Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya
Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi (hayupo pichani).
Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo
na Maji, Amina Makilagi, akizungumza na viongozi wa mradi wa maji wa
Rondo-Mnara na kata ya Mnara.
Ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
wakiwasili kwenye mtambo wa kusukuma maji wa Chikombe.
Mhandisi wa Maji mkoa wa Lindi Valentine Ndyano (aliyevaa shati la
kitenge) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge kuhusu
mtambo wa kusukuma maji.
Msafara wa ziara ukirejea mjini baada ya kukagua mtambo.
Mhandisi wa Maji mkoa wa Lindi Valentine Ndyano akifafanua
jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge kuhusu mtambo wa
kusambaza maji kwenye vituo vya maji.
Kiongozi wa wajube wa kamati akizingumza na wananchi wa kijiji cha
Mnara baada ya kukagua mradi wa maji wa Rondo-Mnara.
Meneja wa Mradi wa Maji wa 7 Towns Upraging Program Kanali
Mstaafu Rajendra Kumar akieleza jambo kuhusu mradi huo.
Wajumbe wakikagua maendeleo ya mradi huo unaotarajiwa
kukamilika Machi mwaka huu.
Meneja wa Mradi wa Maji wa 7 Towns Upraging Program Kanali
Mstaafu Rajendra Kumar, akiashiri jambo wakati alipowatembeza
wajumbe kwenye mradi huo.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment