Msathiki Meya akizungumzia msimamo wake juu ya hatua ya wajumbe wa baraza hilo kutoka nje ya ukumbi wa mikutano wakimtuhumu mkurugenzi wa manispaa hiyo ,Shabani Ntarambe kujihusisha katika uporaji wa Viwanja.
Diwani wa kata ya Kaloleni ,Michael Mwita (CCM) akizungumza juu ya kitendo cha madiwani wenzake kutoka nje huku wakituhumu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhusika katika uporaji wa viwanja vya halmashauri hiyo.
Diwani wa kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akiongozana na mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo kutoka nje ya ukumbi huo.
Mkurugenzi Shabani Ntarambe akitoka ukumbini.
Mstahiki Meya Jafary Michael pamoja na Madiwani wengine wakijaribu kuzungumza na diwani wa kata ya Kilimanjaro Piscus Tarimo aliyebaki ukumbini wakati wenzake wakitoka .
MGOGORO mkubwa umetokea katika kikao cha baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi baada ya Madiwani kususia kikao cha Bajeti ya Manispaa hiyo kilichokuwa kiketi jana, wakitaka iundwe tume ya kuchunguza madai ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Shabani Ntarambe kushiriki katika uporaji wa moja ya kiwanja zilipo ofisi za kata ya
Mawenzi.
Dalili za kutokea kwa mgomo huo zilionekana mapema baada ya kikao cha baraza hilo,chenye utaratibu wa kuanza saa 4 :00 kamili kuchelewa kuanza huku madiwani wakionekana katika viunga vya manispaa hiyo wakiwa katika makundi tofauti wakiendelea na vikao visivyo rasmi.
Majira ya saa 4:20 mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akiwa ameongozana na Naibu Mstahiki Meya Dkt ,Charles Mmbando ,mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Ntarambe waliingia ukumbini na kisha Meya kufungua kwa sara .
Kabla ya Mstahiki Meya Kufungua kikao ,ndipo alipo nyoosha mkono ,Diwani wa kata ya Rau,Peter Kimaro alinyoosha mkono na kuwasilisha hoja kwa niaba ya madiwani wenzake ya kumtaka Meya asifungue kikao.
“Mh Mstahiki Meya ,Jukumu na wajibu wa madiwani ni kutetea na kulinda mali za wananchi vikiwemo viwanja,taarifa sahihi tulizo nazo ni kwamba mkurugenzi Shabani Ntarambe ameshiriki kupora kiwanja zilipo ofisi za kata ya Mawenzi.”alianza kusema Kimaro.
Alisema mkurugenzi huyo ameondoa kwa siri zuio lililowekwa na baraza la halmashauri kwa msajili wa ardhi kwa lengo la kuzia utolewaji wa hati ya kiwanja hicho bila ya kumshirikisha mstahiki Meya na baraza la madiwani.
Kimaro alisema jambo jingine alilofanya mkurugenzi huyo ni kuagiza wataalamu wake kutengeneza hati ya umiliki kwa mtu binafsi na kwamba amedharau agizo la baraza hilo lililotolewa Aprili 17 mwaka jana lililomwagiza kupata hati ya eneo hilo kwa jina la Halmashauri.
“Kwa sababu hizo wajumbe wa baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kupitia Chadema hatuwezi kuendelea na kikao cha baraza mpaka hapo Mstahiki Meya itakapo undwa tume na kuandaa kikao cha baraza cha kujadili kadhia hii.” Alisema Kimaro.
Baada ya Kimaro kumaliza kutoa shutuma hizo ndipo madiwani walisimama isipokuwa wale wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo huku wakiimba na kupiga makofi.
Hata Mkurugenzi (Ntarambe) alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma dhidi yake aligoma kuzungumza na waandishi wa habari akidai kuwa na haraka ya wito katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
“Kwa sasa hatuwezi zungumza chochote kwa ajili ya muda ,naelekea mkuu wa mkoa ameiiita kwa sababu ya suala hili hili,mimi nadhani tupeane muda au muendelee kunisubiri hadi nitoke kwa mkuu wa mkoa takuja tuzungumze”alisema Ntarambe huku akiondoka ofisini kwake na kuwaacha waandishi wa habari.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya wa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwa katika kikao cha baraza la Halmashauri hiyo muda mfupi kabla ya kuvunjika. |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Jafary Michael akijiandaa kufungua kikao ghafla,Diwani wa kata ya Rau Peter Kimaro alismama na kumtaka asifungue kikao hicho. |
Viti vya Waheshimiwa Madiwani vikiwa wazi muda mfupi baada ya kutoka nje ya ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Moshi. |
Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya manispaa hiyo wakiwa wamebaki ndani ya ukumbi wa Halmashauri hiyo mara baada ya madiwani kutoka nje ya ukumbi huo. |
Mkrugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Shabani Ntarambe akijaribu kuzungumzia kitendo kilichofanywa na madiwani hao huku akidai kuwa wamekiuka kanuni za baraza hilo. |
No comments:
Post a Comment