Friday, January 9, 2015

Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya DAWASA wafanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Didas Mwilawi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha akisalimiana na Mwenyekiti wa wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya DAWASA Christine Kilindu alipowasili eneo zinapojengwa ofisi za mradi wa bomba kuu la maji kutoka Ruvu Juu zilizopo Kibaha.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiwa wameanza ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiwa ndani ya tangi la maji eneo la chuo Kikuu cha Dar es salaam wakijionea ukaradati unaoendelea ili kuboresha upatikanajin wa maji jijini.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiangalia maungio ya mradi wa bomba jipya kutoka mtambo wa Ruvu Chini yaliyopo eneo la Mpiji wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Sehemu ya maungio ya mradi wa bomba jipya kutoka mtambo wa Ruvu Chini yaliyopo eneo la Mpiji wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha Mwendapole wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Meneja wa Mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Pintu Dutta kwa kampuni ya VA TECH WABAG kutoka India akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) walipotembelea huo eneo la upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakitembelea sehemu unapofanyika upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiangalia moja ya matangi ya maji sehemu unapofanyika upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu.
Msingi wa moja kati ya matangi matatu yanayojengwa yakiwa ni upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu.
Mafundi wakiendelea na shughuli ya upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu.
Sehemu ya mtambo wa Ruvu Juu kabla ya upanuzi.
Moja ya hatua ya kusafisha maji katika mtambo wa Ruvu Juu kabla ya kusafirishwa tayari kwa matumizi kwa wakazi wa mikoa ya Dar es salaasm na Pwani. (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)

No comments: