Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya watendani wa viwanda jijini Arusha wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi
ya siku moja katika baadhi ya viwanda vya Arusha lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji
wa maagizo ya Serikali kuhusu viwanda kutotumia magogo kama nishati ya uzalishaji
viwandani
Moja ya boiler inayotumia makaa ya mawe katika Kiwanda cha Sunflag. Awali Kiwanda
hicho kilikuwa kinatumia nishati ya Magogo katika shughuli za uzalishaji kiwandani
hapo. Serikali imepiga marufuku matumizi ya magogo ili kuhifadhi mazingira.
Shehena ya magogo iliyobaki katika Kiwanda cha Sunflag. Kiwanda hicho kwa sasa
kimebadilisha matumizi ya nishati ya uzalishaji kutoka kwenye magogo na kutumia
makaa ya mawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Bw. Binesh
Haria Afisa Mwendeshaji wa Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha. Naibu Waziri
alikuwa na ziara ya ukaguzi wa masuala ya Mazingira kiwandani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Arusha Bw. Fidelis Lumato mara baada ya kutembelea kiwanda cha
A –Z cha Jijini hapo kukagua masuala ya Mazingira.
No comments:
Post a Comment