Na matukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amechangia kiasi cha Tsh
milioni 15 kwa ajili ya ukarabati wa kanisa la Roman Katoriki
parokia ya Madunda wilayani Ludewa pamoja na kusaidia vinanda
viwili kwa kwaya mbili kanisani hapo.
Akikabidhi
msaada huo leo mara baada ya ibada ya jumapili mbunge
Filikunjombe alisema kuwa amefika kanisani hapo baada ya kuomba
kinada na kwaya ya kanisa hilo na hivyo kutokana na kuwepo kwa
kwaya mbili amelazimika kutoa msaada wa vinanda kwa kwaya zote
pamoja na kusaidia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa
kanisa hilo.
Kwani
alisema kuwa kanisa hilo ni mmoja kati ya makanisa makongwe
yaliyojengwa miaka ya 1980 katika wilaya hiyo ya Ludewa na kuwa
kanisa hilo ndilo kanisa la tatu kujengwa kwa wilaya ya Ludewa
hivyo linahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kuendelea
kuwafanya waumini wa kanisa hilo kupata eneo la kuabudia.
Filikunjombe
aliwataka waamuni hao na waumini wa madhehebu mengine katika
wilaya ya Ludewa kuendelea kumwombea afya njema ili kupata nguvu
ya kuwaletea maendeleo kama ambavyo ameendelea kufanya katika
wilaya hiyo kama njia ya kuwashukuru wananchi wake kwa
kumwamini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa kumchagua kuwa
mbunge wa jimbo hilo la Ludewa .
"Imani
ambayo wenzangu wananchi wa Ludewa mlioionyesha mwaka 2010 katika
uchaguzi mkuu kwa kunichagua kuwa mbunge kamwe sitaacha
kuwakumbuka wananchi wangu wa Ludewa kila ninapokuwa bungeni
mawazo yangu kurejesha ahsante yangu kwangu na kuona wilaya yetu
ya Ludewa inaendelea kupiga hatua"
Pia
mbunge huyo alisema kwa sasa mkakati wake na wa serikali ya
Rais Dr Jakaya Kikwete ni kuona ujenzi wa barabara ya lami
kutoka Njombe hadi Ludewa inajengwa na tayari wakandarasi wa
kuanza ujenzi huo wamekwisha patikana ndani ya miaka hii miwili
bararabara hiyo itakuwa imejengwa na ujenzi wake utafanyika kwa
awamu tofauti.
Hata
hivyo alisema kuwa akiwa mbunge wa jimbo hilo kamwe hatakubali
kuona wana Ludewa anawapelekea maendeleo kwa upendeleo na kuwa
lazima pande zote ikiwemo la milimani , mwambao wote wananufaika na
matonda yake kwa kuwa na maendeleo wote.
Kwa upande wake katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akimpongeza mbunge huyo kwa kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya jimbo hilo ,alisema kuwa kazi zinazofanywa na mbunge huyo zimekipatia heshima chama cha mapinduzi (CCM) na kuwa utendaji mzuri wa kazi wa mbunge huyo ndio ambao umeitangaza wilaya ya Ludewa .
|
No comments:
Post a Comment