Thursday, January 15, 2015

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO JIMBO LA MPENDAE,MKOA WA MJINI MAGHARIBI

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho,waliofika kwa wingi katika mkutano wa hadhara,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.Ndugu Kinana kabla ya kuhitimisha ziara hiyo alishiriki kazi za kijamii na kukagua miradi mbalimbali ya chama.
katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho,waliofika kwa wingi katika mkutano wa hadhara,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.Nape pia aliipongeza kazi nzuri inayofanywa na Dkt shein ya kuimarisha chama,amewataka viongozi mbalimbali wa chama hicho kuiga mfano wake,pia amewataka viongozi wa chama hicho kuacha kuwa na majivuno badala yake watoke na kukutana na wananchi kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo yao kwa namna moja ama nyingine.

 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,Jimbo la Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa wilaya ya Mpendae na wanachama wa CCM wa jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani,Mkoa wa Mjini Magharibi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,mkoa wa Mjini Magharibi.
 Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Binti Amrani Mpendae,Wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi jioni ya leo.

 Sehemu ya Meza Kuu.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Vuai Ali Vuai akisoma baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye katika inayopendekezwa mbele ya wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara,uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Binti Amrani Mpendae,Wilaya ya Amani,mkoa wa Mjini Magharibi.
 Sehemu ya umati wa Wakazi wa wilaya ya Mpendae katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani,Mkoa wa Mjini Magharibi wakifautilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,Jimbo la Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi.
 katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwalisha kiapo baadhi ya wanachama wapya walijiunga na chama hicho sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
 Sehemu ya viongozi mbalimbali wa chama cha CCM wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa Binti Amrani Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.
 Wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Mlezi wa mkoa wa Mjini Magharibi na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mara baada ya msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kuwasili mkoa wa Mjini Magharibi.




 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua Ofisi ya Tawi la CCM Nyerere B,katika Wilaya ya Amani,ndani ya Jimbo la Magomeni Mkoa wa Mjini Magharibi



 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipiga makofi mara baada ya kushiriki ujenzi na uzinduzi wa Ofisi ya tawi la CCM-Kilimahewa Juu,ambalo lilichomwa moto na kuvunjwa kabisa wakati wa harakati za kundi la Muamsho katika jimbo la Amani
 Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukikatiza katika mtaa wa Daraja Bovu wakati wakielekea kuzindua na kushiriki ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Kiungani. katika jimbo la Chumbuni,Wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.
 Mbunge wa Chumbuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Pereira Ame Silima akizungumza jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto aliposhiriki ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Kiungani.







  Mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.Salim Hassan Abdullah Turky  akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakati alipowasili katika jimbo la Mpendae mapema leo katika wilaya ya Amani Mkoa wa Mjini Magharib,ambapo pia alipokea taarifa taarifa ya kazi za chama na Serikali,kuzindua ukumbi wa mikutano wa Jimbo pamoja na kukabidhi Vyarahani na Kompyuta kwa vijana wa jimbo la Mpendae.
 Mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.Salim Hassan Abdullah Turky  akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Amani,katika jimbo la Mpendae mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Amani,katika jimbo la Mpendae mapema leo asubuhi,ambapo pia alipokea taarifa taarifa ya kazi za chama na Serikali,kuzindua ukumbi wa mikutano wa Jimbo pamoja na kukabidhi Vyarahani na Kompyuta kwa vijana wa jimbo la Mpendae.

No comments: