Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu akielekea katika
kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama
hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105
waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani
Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani
tuheshimiane.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Vijana wapatao 105 waliokuwa
chama cha CUF na kuhamia CCM.Wakisoma taarifa yao kwa Ndugu Kinana
walieleza manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF,walieleza
kuwa tangu wamehama chama hicho wamekuwa wakibugudhiwa na kufanyiwa
fujo kiasi ambacho wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kimaendeleo
ikiwemo na shughuli zao za uvuvi kusimama,hivyo wamemuomba Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana kulishughulikia jambo hilo ili waweze kuendelea na
shughuli zao bila kubugudhiwa kwani wanataka kuishi kwa amani na
utulivu.
Akizungumza Ndugu Kinana alisema kuwa chama cha CUF
hakitendi haki katika suala zima la demokrasia, ''kwani kila mtu ana
uhuru wa kuhamia chama anachotaka na haitaji kubugudhiwa,hivyo Viongozi
wa CUF,wanapaswa kulitambua hilo na kuwaacha wananchi waamue watakavyo
ili mradi hawavunji sheria za nchi wala kumbugudhi mtu'' alisema Kinana.
Kinana
yupo katika ziara ya siku tano ya Kikazi kisiwani Pemba,akihimiza na
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni
pamoja na kukagua uhai wa chama kisiwani humo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa Maskani ya tawi la CCM-Tuheshimiane katika kijiji cha Mnarani Makangale,Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
Baadhi
akina mama Wakulima wa Mpunga wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana aliyekwenda Bonde la Mpunga Koowe kuangalia na
kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.
Pichani
kati ni Afisa Mkuu wa Idara ya Umwagiliaji maji-Pemba Mbarouk Ali Mgau
akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda bonde la Mpunga Koowe-wingwi, kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.Afisa Mbarouk alieleza kuwa mradi huo umegharibu kiasi cha shilingi Milioni 170 zilizotolewa na TASAF.
Ndugu
Kinana akiwa na baadhi akina Mama ambao ni wakulima wa zao la Mpunga
katika Bonde la Koowe,wakishiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi
katika bonde hilo
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimia na Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni,Dkt.Rashid Daud mara baada ya kuwasili katika hospitali ya
Wilaya ya Micheweni,Kaskaini pemba mapema leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizingumza na baadhi ya Madaktari wa hospitali ya Wilaya ya
Micheweni,mara baada ya kuwasili katika hospitali hiyo,Kaskazini Pemba mapema leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya
Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba, wanaoshuhudia ni madaktari viongozi
mbalimbali wa wilaya ya Micheweni na hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akipata maelezo kutoka kwa Dkt.Rashid Daud Mkasha Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Micheweni wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa wodi katika
hospitali hiyo.
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Majenzi mjini Micheweni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kweny uwanja wa Majenzi mjini Micheweni.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi
wa chama cha CCM,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Shaame
Mata,Wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba mapema leo.Pichani
kulia ni Mbunge wa Viti maalum Pemba,Mh Maida Hamad Abdalllah na kushoto
ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndugu Vuai Ali Vuai.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba
No comments:
Post a Comment